Hivi, huwa ukiongea peke yako unaongea na nani?

muda mwingine kuna sauti toka ndani ndio inaongea na wewe, na hii sauti ya ndani huwa inakuwa na mvutano kwa mfano kabla ya kufanya jambo ambalo unasita huwa kuna sauti moja inakuambia fanya nyingine inakuambia usifanye, ushawahi kukutana na hilo ndugu mshana?
The conservation within oneself ndio maana nikasema kuna hasi na chanya ndani ya nafsi
Hasi inamwakilisha shetani na mambo yote mabaya
Chanya inamwakilisha Mungu na mambo yote mema
Maamuzi yatakayotokana na hayo mazungumzo itategemea ulimpa ushindi nani Mungu ama shetani?
 
Asante MSHANA JR...ila nimefurahi kuona wale wanaokuita WAKALA WA SHETANI hawajatia maguu hapa.
Baada ya kazi ngumu mno ya kuwafafanulia kwa upole hatimaye wamenielewa
 
Mkuu nimeona matunda ya kuongea na mimi mwenyewe baada ya kuwa nasoma vitabu vya motivation na nimejikuta my subconscious mind kweli inapick na kusajili ninavojiambia na hivyo kuniongoza kwenye kufanya mambo yenye matokeo yanayoonekana. Kila asubuhi au jioni nikitoka mazoezini kukimbia huwa naanza kujiambia mwenyewe nini napaswa kufanya ili nifike mbali. Na hapo huwa natumia muda huo kusali na kujiombea mimi na familia yangu. Hakika naona matokeo ya kujiongelesha mwenyewe.
 
Ni ushuhuda mzuri umepata ufunuo mwema, Mungu zaidi kukuongoza
 
Nikiwa na jambo linalo nisumbua huwa naongea mwenyewe kimyakimya ila kuna wakati huwa natoa mguno kwa sauti, mpaka mtu wa pembeni anauliza ni nini? Au umeona nini? Lakini wakati naongea na nafsi yangu huwa kimya kimya na mara nyingi hunisaidia kufikia maamuzi yanayo nisaidia bila hata kumshirikisha mtu mwingine, napata ahueni kabisa.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] miguno ni dalili kwamba umehama ulimwengu
 
Haaahaa, nipo ulimwenguni mkuu, but ninashangaaa kwa nini siwezi kuacha kuguna au kuguna kimyakimya kama ninvyo waza.
Ni yale mazungumzo yanahama kutoka ndani na kuleta uhalisia wa sauti
 
Du! halafu nina jambo lingine ambalo huwa lina nishangaza sana ninaweza kukaa gafla mawazo yakahama nikamkumbuka mtu nilie potezana nae kitambo sana, nikisha muwaza u haipiti siku mbili lazima nikutane nae au nipate habari zake, wakati mwingine ninapanga jambo kufikiria jinsi ya kulifanya baada ya muda mfupi lile jambo linapatiwa ufumbuzi kwa jinsi nilivyo kuwa nawaz ila naogopa kulisema mbele ya jamii, huwa nawaza nina jini au?
 
Ni nguvu iliyoko ndani ya ufahamu ni nguvu ya uvutano na kufanya vitu vitokee lakini yako iko kwenye level ya chini , level inayofuata ni machale halafu baada ya hapo ndio inaingia kwenye uwezo wa kutabiri
Hizo nguvu tunazo ni haya makandokando tu yaliyouzonga ufahamu wetu ndio maana zinashindwa kufanya kazi kwa ukamilifu na utimilifu
 
Huwa nawza sana na wakati mwingine naogopa mkuu, unamkumbuka mtu usiku bila kuwa na shughuli nae yoyote halafu asubuhi unaelekea kwenye shughuli zako unakutana nae, inaogopesha sana. Ila Mungu ana maajabu yake kwa sie viumbe vyake.
 
Hapana huna haja ya kuogopa kwakuwa hiyo nguvu uliyonayo wewe inafanya kazi positively
Nilishawahi kukutana na dada mmoja nadhani alikuwa na kitu kingine kikubwa na kibaya zaidi huyo akiota kuwa fulani kafa au kapata ajali ujue hilo lazima litokee
 
Huwa nawza sana na wakati mwingine naogopa mkuu, unamkumbuka mtu usiku bila kuwa na shughuli nae yoyote halafu asubuhi unaelekea kwenye shughuli zako unakutana nae, inaogopesha sana. Ila Mungu ana maajabu yake kwa sie viumbe vyake.
mie pia kuna kitu kimeshanitokea zaidi ya mara nne hivi,unakuta kwenye simu yako una namba za jamaa zako hamuwasiliani kwa muda mrefu sana,mwisho unaamua kuzifuta,ukifuta tu jamaa ndio wanaanza kukupigia ukiuliza nani mbona imekuja namba ngeni?anajitambulisha jamaa ulofuta namba yake jana tu au asubuhi hiyo,hii huwaga ni nini eti?naamini sio peke yangu hii incidence hunitokeaga..
 
Back
Top Bottom