Bulaya001
JF-Expert Member
- Dec 21, 2018
- 5,987
- 6,682
- Thread starter
-
- #21
Pole sanahawa wadudu waliwahi kunipa tabu sana mwaka 2013 nilipokuwa nasafiri na basi la mohamed trans la dar - bukoba
ni katika kile kipindi ambacho mabasi ya mohamed trans yalikuwa yanaenda ukingoni kufa, wahusika walikuwa hawapulizi dawa.
mziki ulianzia kahama mida ya usiku. basi zote zilizokuwa zinatoka dar kwenda bukoba ziliamliwa zilale kahama ili alfajiri ziamshe kuendelea na safari.
baadhi ya abiria waliamua kwenda kulala lodge za jirani na pale stendi na sisi wengine tukakomaa kwa kulala ndani ya basi.basi weee acha tu. kunguni walitufanya kitu mbaya sana. hakuna abiria aliyelala.
ilikuwa ni fulu kujikuna....ikabidi nitoke nje nikaenda kukaa na madereva bodaboda nikipiga nao story mpaka asubihi.