Hivi huwaga unafanyaje; Pesa ya kodi inakaribia na hauna kitu daaah!

Hivi huwaga unafanyaje; Pesa ya kodi inakaribia na hauna kitu daaah!

hamza mahundu

Member
Joined
Dec 20, 2018
Posts
58
Reaction score
116
Kuna mazingira kama haya, umekopa pesa kwa mtu uizungushe ikaferi, matarajio ulipe Kodi, mama mwenye nyumba ulishamuahidi MWEZI WA 10 tarehe 18 unampatia pesa yake leo tarehe 2. Aiseeee na ingebidi MWEZI uliopota umalize deni.

Maokoto zero kula kwenyewe kumekuwa kwa tabu saaana, kulala njaa kawaida.

Fikiria ni wewe? Unajitoaje hapo
 
Ongeanae asipokubali turudi hapo kwenye unajitoaje...
 
Ukiona upo sehemu utaftaji wako unafeli mpka hela ya kula ondoka katafute maisha sehemu nyingine asilimia kubwa tunawashauri wakajipange mbali na hapo unatafuta kudhalilika.

Na ukijipata sio lazima ukae sehemu yenye kodi kubwa jibane ukiweza kujenga hayo mambo mengine hutasumbuka nayo. Ushauri kwa sisi maskini ni bora ujenge kuepuka dharau na masimango ya wenye nyumba.
 
Nenda kwenye zile nyumba ambazo zipo pembeni ya mji kidogo unakuta imejengwa bado kumalizia vitu vidogo vidogo, unakaa humo wakati unajitafuta
 
Mara ya kwanza niliona baba mwenye nyumba mkuda sana.

Ila Sasa naelewa kuwa baba mwenye nyumba Huwa anajisikiaje akiambia na mpangaji aisee Sina kitu mpaka mwezi wa 11
 
Cha msingi Anza kujipenda mwenyewe kama una fedha kidogo usilipe deni endelea kumantain bajeti yako kwenye mahitaji yako muhimu... Kua muawazi Kwa mama mwenye nyumba kwani maisha ni maji kupwa maji kujaa.
Nb. USILIPE DENI KAMA UNA FEDHA KIDOGO
 
Tatizo la wabondo huwa atu calculate tu coz unakuta mtu anakaa chumba kwa mwezi elfu 30 nisawa nakulipa buku kila siku na katika miangaiko yake anauwezo wakupata elfu 17 per day kima chachini lakini mwisho wa siku unakuta eti unaleteawa nots
 
Kuna mazingira kama haya, umekopa pesa kwa mtu uizungushe ikaferi, matarajio ulipe Kodi, mama mwenye nyumba ulishamuahidi MWEZI WA 10 tarehe 18 unampatia pesa yake..Leo tarehe 2. Aiseeee. Na ingebidi MWEZI uliopota umalize deni.

Maokoto zero.kula kwenyew kumekuwa kwa tabu saaana,kulala njaa kawaida.
Fikiria ni wewe?? Unajitoaje happoo
Usikate tamaa ndugu bado una wiki mbili lolote linaweza kutokea.
 
Back
Top Bottom