Ha ha ha hii topic imenichekesha balaa.....WAnaume bwana wananichekesha sana, unaweza ukampenda kweli, yani kweli kweli, na kwa kuwa ni rafiki yako unajua unakuwa umemzoea, yani kuna vihistoria na vistori ambavyo vinawaunganisha, achilia mbali hisia za kimapenzi.
Sasa kwa mdada ambaye ni muwazi na anapenda kuongea anaweza akajikuta tu anasema halafu unajua mi nakupendaga, tena nakupendea hiki hiki na hiki. Kama utani lakini kweli. Na ujue kwa hakika mdada aliyekuzoea akitamka hilo neno ujue amemaanisha sana. Kipo moyoni hicho kitu...Moyo unampasuka.
Wanaume sasa, looh huyu demu ananitaka, na kwenye vijiwe vya bia akifika stori ndiyo hiyo, analishwa humo weeeeh, demu atakutokea je wewe, kwanza yule demu hivi na hivi, makasoro kibao mnamtoa......Ukitoka hapo kumbe limoyo linakuuma NAMPENDA huyu dada lakini................he he he
Ujue msichana anapokuambia hivyo we unajifanya kumpotezea, anaumia, anajistukia, anajisikia vibaya sana....Hivi mimi kwa kwa nini hata nimemwambia, hivi kanionaje, loooh nimkimbie au nifanye nini, nitathubutu kuongea naye tena? Na mengine kibao yanamsumbua kiakili, kiroho na kimwili. Kwa sababu hakutegemea awe na ujasiri na uhuru kiasi hicho kwako halafu akutane na hicho ulichompatia.
Sasa basi kinachofuata baada ya hayo yote.....anajitahidi kuikataa ile hali, nakujisahaulisha. Kwa nguvu sana, hata kwa machozi. Siku akisema It's OVER...To hell........kwani yupo peke ake? Ndio basi, amefanya maamuzi magumu, na kwa bahati mbaya atokee mtu amuonyeshe upendo..........WE UNAKUJA KUSTUKA...unaona manyoya.
Acheni usharobaro..............Angalia maisha katika uhalisia wake kutoka kwenye huo uhalisi kuliko kawaida kawaida hii....na huu u-artificial artificial tunauwekaga kwenye maisha....................TUTAPOTEZA VILIVYO VYEMA