Hivi huyu Chef anayeonekana kwenye kipindi cha Jambo huwa na jukumu gani?

Hivi huyu Chef anayeonekana kwenye kipindi cha Jambo huwa na jukumu gani?

simakoku

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
537
Reaction score
586
Huwa namuona chef mmoja anaonekana kwenye kipindi cha jambo Tanzania kila asubuhi kwanye TBC.

Huwa ana jukumu gani? Sijawahi kuangalia hicho kipindi mpaka mwisho, ila kwa myda niliopata kuangalia sijawahi kumuona hata akiwahudumia watu hivyo anavyopikaga.

Mfano leo angalau nimepata nafasi ya kuangalia jambo, namuonactu mara akate matunda, sasa hivi namuona yupo busy anakanda maandazi.
 
Baba ntilie/mama ntilie huyo (sina hakika maana sijawahi angalia TBC).

Anakaanga vitu vya kwenda kuuza.

Wewe angalia kipindi, muache msela akarangize madikodiko yake.
 
Huwa namuona chef mmoja anaonekana kwenye kipindi cha jambo Tanzania kila asubuhi kwanye TBC...
Si uangalie kipindi kizima? Huangaliagi halafu unataka kujua! Au ndio mkumbo wa " mie sitazamagi tbc"? Acha uzembe tizama tv ya taifa
 
Kipindi ni kizuri achen kujishaua hapa, tatizo mmezoea watangazaji wenu wanao piga piga makelele kama wakina baba level. Watu wapo professional pale. Na yule kaka mpishi kuna muda huwa anaelezea aina ya pishi analopika sisi tunaopika tunajifunza mapishi
 
Pale DSTV wakishafanya yao hakuna namna zaidi ya kuangalia TBC [emoji1].... wewe kaa hadi mwisho umtazame akifanyacho unavunga hujui wakati unajua
 
Mnaovunga hamuangalii TBC ndiyo nyie wkt wa kombe la dunia mlishinda kwenye hiyo channel kutwa mzima leo mnaponda ahahhaaa.
Hawa jamaa huwa wanachekesha sana🤣🤣, halafu kwa akili yake anadhani akisema huwa haangalii TBC tutamuona ndio ana IQ kama ya Einstein
 
Back
Top Bottom