jide anapaswa kuheshimu mashabiki wake...na wapotoshaji waache kumshauri vibaya ili aendeleze kiburi...
Kama ana matatizo na waandaaji wa tuzo bado hana sababu ya kuhamishia matatizo kwa mashabiki wake.......
Kuuliza kuwa tuzo zimeshafanyika ? Ili hali alipigiwa kura na kusubiriwa na mashabiki wake ili kushare naye furaha ya kupata tuzo...ina maana alimaanisha waliompigia kura na kumsubiri wamuone jukwaani hawakuwa na kazi ya kufanya... Haikuwa uungwana hata kidogo...
Angeonyesha uungwana hata mara tu baada ya zile tuzo kwa kuwashukuru mashabiki na kuomba radhi kwa kutokuwepo ukumbini...na kama angeona inafaa pia angeweza kuweka wazi kuwa labda haridhishwi na waandaaji wa kili music awards.
Walisema waswahili......heshima ni kitu cha bure.....