Hivi huyu mtu anayejiita Mfalme Zumaridi anatuchukuliaje?

Mssiingilie imani za watu, Wachungaji wangapi wanasema kuwa wanazungumza na Mungu?... wangapi wanasema wamepewa Ufunuo na mbona hawabughudhiwi?

Huyu naye ni mfalme na ni mtume, so kimahesabu anazungumza na mungu (KWA IMANI YAO NA WAFUASI WAKE)

Muacheni msimbughudhi mfalme,
Acheni asongeshe Injili, Hata imani yenu kwa wengine inaonekana kituko.....
 
Nakazia mkuu
 
Nani alimuona Yesu na kuthibitisha hayo uliyoandika kuhusu yeye tofauti na kusoma kwenye vitabu?
Hivyo hivyo nani alimuona Muhammad na kuthibitisha maisha yake zaidi ya kusoma kwenye vitabu?

Nani alikufa akaenda Mbinguni na kuona kulivyo akarudi na kusimulia aliyoyaona zaidi ya kusoma kwenye vitabu?

Mbinguni kumeelezwa kuna Pepo na Moto, huko Peponi watu watasifu na kuabudu, wengine watakutana na mito ya maziwa na asali, na huko Motoni ni kuunguzwa na watu watapewa maji ya usaha,

Hayo yote tunaamini hadi kuogopa kabisa bila kua na uthibitisho wowote, je na sisi ni Wagonjwa wa Akili?
 
Umenena,
Kila Mtu huona Imani ya mwenzie ni kituko lakini kama kila Mtu angeheshimu imani ya mwenzie na kushika yake, huu uzi usingekuwepo,

Nimeuliza kwanini kwa Zumaridi iwe ana tatizo la akili lakini kwa Wachungaji wengine wawe mashujaa?
 
Sawa
 
Mi nadhani swali hilo ungewauliza makerubi wake wanaomwamini kwamba ni Mfalme wa mbinguni
 
Huyu dada inaonekana hata anapoishi kutakuwa na mazingaombwe mengi sana...
 
Muwe mnamulewa, Mbinguni anayozungumzia yeye ni kileleni...

Na kwa miuno yake kwa nini asifike...
 
2mia akili,huyo alipokuwa ndani,amepewa maagizo na systeam kwamba akiachiwa akirudi uraiani ajimalize ili huduma yake ife.....apotee
 
Zumaridi ni sawa tu na Kuhani wetu anayesema Yesu huwa anamtokea kabisa na kumpa maelekezo ya Ibada za kufanya... πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hata Dominic naye alitwambia alipewa Rozari eti ...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nailaumu hii serikali ya mama yenye mwelekeo ule wa kibepari 'custumer beware' wakati ikijua wananchi wengi bado ni wajinga. Serikali hii itambue vita dhidi ya ujinga ni jukumu la serikali kwa hivyo inabidi kuwalinda wananchi wanapokabiliwa na mafisadi kupitia imani za kiroho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…