Hivi huyu Vandernbroeck anatutafuta nini Wanamsimbazi?

....aisee, umeongea vzr sana ndugu...no more no less...
 
Naamini unatania. Huwezi ukapindua kwa kupanga striker mmoja mbele. Jamaa wakija na game plan kama ya jana na tukafanya ujinga wa

[emoji16][emoji16] Naamini unatania. Huwezi ukapindua kwa kupanga striker mmoja mbele. Jamaa wakija na game plan kama ya jana na tukafanya ujinga wa kuweka striker mmoja tumekwisha.
Naitania tu hii familia ya MO,Tatzo wanacheza kwa mazoea sana na yote hii inasababishwa na mdomo wa Manara🀣🀣🀣🀣🀣
 
Ndo bongo tulivo.. Yan kuwa kocha wa timu za bongo ni kazi kweli kweli..

Hayo ni matokeo tu kama ambavyo mpira ulivyo na matokeo matatu.. Imagine Simba Jana angeshinda sidhan kama Leo ungeandika Uzi wa kocha kutimuliwa.

Yani Simba kila game tushinde tumekuwa nani kwa mfano? Hata wapinzani nao wanakuwa na tactic na lengo la kushinda kikubwa team ijiandae kwa game ijayo..
 
Pamoja na kufungwa lawama hazikosekana kwenye Moira ila naona mechi ijayo mambo yanaweza yakawa mazuri,ijitahidi tu kuwafungua wapinzani pindi wakidifensi
 
USAJILI MBOVU WA WACHEZAJI UNAIGHALIM SANA SIMBA.

HAMASA IPO CHINI SANA NDANI YA TIMU.
 
Unataka kusema kufungwa ni halali yetu?

Sasa kwanini timu inahangaika kulipa wachezaji na benchi la ufundi ili wafanye vizuri kwenye mashindano mbalimbali?

Tunatakiwa kuwapressurise wahusika ili timu ifanye vizuri. Tena benchi la ufundi na wachezaji wanatubore sana sisi mashabiki wasipocheza vizuri na kushinda .
 
unhangaika hata kujibu ya nini?shida ya kishingo inajulikana ni mbabaishaji ana plan moja tu team ikibanwa kwisha kazi hata wazimbabwe walishaliona hilo, alivovurunda na kmc watetezi wakasema alikuwa anawazuga platnum sababu walituma mashushushu dsm ,

jana wamekuja na mengine kwamba tukubaliane na matokeo MATATU,NDIYO MAANA MASHABIKI WA SIMBA WANAACHA KWENDA UWANJANI SIKU HIZI, suala siyo kufungwa,teams inaweza ikafungwa lakini inapambana na kocha anaonekana kuna kitu anatafuta siyo huyu boya

Simba ya sasa ni simple sana kuwafunga wee waache wapigiane pasi za nyuma na pembeni sababu wako slow ukipata mipira ipitishe katikati kwa speed kubwa kama siyo mkude kukuchezea rafu kule nyuma kwa wawa na na onyango unawapita kirahisi sana

halafu wala haina shida kujua formation yao ni 4-2-3-1 kuanzia mwanzo wa msimu hadi mwisho,haijalishi wanacheza na majimaji au tp mazembe,wako nyumbani au ugenini,kishingo keshakariri hivyo maskini ya Mungu anaonekana ni kocha cheap sana ..wtf
 
Kufungwa si halali lakini ni matokeo ya mpira hilo halina lawama kwa kocha.
Na wachezaji kulipwa vizur pia sio guarantee ya kutokufungwa, kumbuka hata wapinzani nao walikuwa wanataka matokeo na wamepata..

Kwa iyo sisi tukubali kwamba tumepoteza mchezo na wachezaji wajiandae kwa match inayofata nafasi bado tunayo ..
Hayo ya kocha afukuzwe haya aletwe kocha gani ambaye kila match kwake itakuwa ya ushindi dhidi ya wapinzani? Kocha wa Namna hiyo hayupo..

Mashabiki ifikie wakati tubadilike na tukubali matokeo sio kila game tukipoteza bas tunatafta makosa na lawama kwa makocha.. Nadhani yule kocha mzungu wa Yanga aliyeondoka aliacha ujumbe mzuri kabisa kwa mashabiki wa bongo mkamuona mbaguzi..

Na match ijayo hata tukishinda naomba uendelee kushinikiza kocha afukuzwe ili nyuzi hizi zisiwepo tu Simba wakifungwa..
 
malalmiko dhidi ya kishingo yako wazi kabisa ila mna twist na kuja ana angle yenu,kila la kheri bwana tushachoka siye acha tunyamaze tusiojua mpira utaona mechi na majimaji kombe la FA kama hajaanza 4-2-3-1 hata akicheza na team ya ndondo yeye ni hivyohivyo unaamini team kama simba ni ya kucheza mfumo mmoja msimu mzima,HADI SASA TUSHAKUWA UNDER DOGS KWA UTOPOLO NA YULE JAMAA WAO CEDRIC KAZE ALIVYO SMART WA KUHAMISHA HATA FORMATION TATU MCHEZO MMOJA TUSUBIRIE VIPIGO TU HUKU MKITETEA KISHINGO WENU
 
Tempo ya team imeshuka sana,jiulize kwa nini team iliwahi kutoka congo na misri ikiwa imekula 5-5 lakini watu walikuwa very optimistic wakisema kwa mkapa hatoki mtu au nkana alitufinga 2-1 kwao na bado tukawa na imani na uchebe?
Team ilikuwa inatembea kwelikweli kule mbele kuna okwi-boko-kagere lakini jana goal moja tu tuna wasiwasi na tuna haki ya kuwa na wasiwasi
kishingo kwanza wakampime akili mimi nahisi ni Taahira au teja la heroine
 
Hivi wewe ukocha ulisomea wapi?
 
Inaonekana wewe ni munufaika na uwepo wa huyo kocha. Kocha amekuwa na game plan ile ile muda mrefu kiasi kwamba hata wapinzani wamekuwa wepesi kutusoma na kutudhibiti. Kiasi kwamba mfumo wake 4-2-3-1 umezoleta na yeye habadiriki haraka. Siku za hivi karibuni timu imekuwa ikipata matokeo kwa taabu sana hata ikicheza na vitimu vidogo vidogo. Halafu unakuja hapa kumtetea Kocha.
 
Uko sahihi sana. Inaonekana hajui hate kuwapa hamasa wachezaji wake yeye kama mwalimu/kocha.
 
Mkuu acha kupanic kijinga cz mpira una matokeo matatu..tatizo sisi mashabiki hatutakagi matokeo mengine zaidi ya ushindi! Na timu ikishinda huwez kuskia kocha akisemwa ila itoe sare au kufungwa lawama zote anabebeshwa kocha acheni hizo jamani, lakini pia mkumbuke wachezaji ndio hawahawa asilimia kubwa wametumika kwa muda mrf na huu ni wakati viwango vyao kushuka ama kuchoka na kasi kupungua naturally..kuna wakati tukubaliane na hali halisi na kocha anafanya kazi yake vzr tu na tumpe ushirikiano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…