Hivi huyu Vandernbroeck anatutafuta nini Wanamsimbazi?

Hivi huyu Vandernbroeck anatutafuta nini Wanamsimbazi?

Nimetizama uchambuzi wa Azam tv kwa kweli pale hakuna kocha, naamini huyu kocha anazidiwa uwezo na seleman matola tena na makocha wengi wa bongo, sema sisi watu weusi tatizo letu tunaabudu sana ngozi nyeupe.
 
Basi mimi ni mtu pekee niliyemkataa kocha hata baada ya ushindi wa goli 3.

Timu ina wachezaji wenye vipaji vikubwa sana lakini tatizo linaonekana ni mwamuzi.

Mpira uko na pace ya chini mno kiasi kwamba kwamba kupata matokeo,kunategemea timu unayocheza nayo wasiwe na morali pia.Ukikutana hata na timu ya daraja la 3 yenye morali huwezi shinda kwa kasi ile ya mpira.

Hatuingilii kazi ya mwalimu lakini tunaona amekosa mbinu mpya kuvitumia vipaji vilivyopo
Mkuu acha kupanic kijinga cz mpira una matokeo matatu..tatizo sisi mashabiki hatutakagi matokeo mengine zaidi ya ushindi! Na timu ikishinda huwez kuskia kocha akisemwa ila itoe sare au kufungwa lawama zote anabebeshwa kocha acheni hizo jamani, lakini pia mkumbuke wachezaji ndio hawahawa asilimia kubwa wametumika kwa muda mrf na huu ni wakati viwango vyao kushuka ama kuchoka na kasi kupungua naturally..kuna wakati tukubaliane na hali halisi na kocha anafanya kazi yake vzr tu na tumpe ushirikiano!
 
Jana ameiangamiza timu yetu, jana ametuumiza Wanasimba. Na hii si mara yake ya kwanza kutufanyia hivi.

Wale Platinum FC kwa jinsi nilivyowaona si wakali sana wa kututisha (najua game ijayo tutapindua matokeo) ila game plan ya Mwalimu wetu na zile sub zake za hovyo ndo zilizotugharimu. Kulikuwa kuna haja gani ya kumtoa Meddie Kagere badala ya kumwongezea nguvu? Kuna watu watasema "usimwingilie Kocha,yeye ni mtaalamu anajua zaidi kuliko wewe shabiki", acheni ujinga! Mmeambiwa wataalamu huwa hawakosei na sometimes kuzidiwa na amateurs?

Nauliza; kocha una chuki gani dhidi ya Kagere ambaye alikuwa anaisumbua Platinum kuliko yule mchovu Mugalu aliyeingia? Halafu unampendea nini Mzamiru Yassin na kiwango chake kile kibovu? Huyu Miraji Athumani ni mzuri, lakini kwakuwa umekuwa humpi nafasi, unadhani angefanya nini cha ajabu jana?

Nakuambia anza kupanga nguo zako kwenye begi. Kwanza ulikuja ukiwa kimbaumbau,una koromeo refu na macho kama una utitiri wa kuku. Sasa tumekulisha ukanawiri na ukajua kuvaa halafu unaanza kutuzingua. Get prepared!
Tatzo sio coach tatizo wachezaji mkuu wamekosa Sana magoli

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Kwako GENTAMYCINE anasemaje🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ndo bongo tulivo.. Yan kuwa kocha wa timu za bongo ni kazi kweli kweli..

Hayo ni matokeo tu kama ambavyo mpira ulivyo na matokeo matatu.. Imagine Simba Jana angeshinda sidhan kama Leo ungeandika Uzi wa kocha kutimuliwa.

Yani Simba kila game tushinde tumekuwa nani kwa mfano? Hata wapinzani nao wanakuwa na tactic na lengo la kushinda kikubwa team ijiandae kwa game ijayo..
Hakuna aliyesema tunataka tuwe tunashinda game zote daima, ila pia hakuna shabiki aliye tayari kuona timu inapata matokeo kwa bahati nasibu au kufungwa kizembe zembe.

Hivi umefatilia performance ya Simba kwenye hizi game tatu za mwisho (mbili za VPL na hii ya CL) ? Hii Simba inayowatia pressure mashabiki wake wenyewe wewe unaona iko sawa?
unhangaika hata kujibu ya nini?shida ya kishingo inajulikana ni mbabaishaji ana plan moja tu team ikibanwa kwisha kazi hata wazimbabwe walishaliona hilo, alivovurunda na kmc watetezi wakasema alikuwa anawazuga platnum sababu walituma mashushushu dsm ,

jana wamekuja na mengine kwamba tukubaliane na matokeo MATATU,NDIYO MAANA MASHABIKI WA SIMBA WANAACHA KWENDA UWANJANI SIKU HIZI, suala siyo kufungwa,teams inaweza ikafungwa lakini inapambana na kocha anaonekana kuna kitu anatafuta siyo huyu boya

Simba ya sasa ni simple sana kuwafunga wee waache wapigiane pasi za nyuma na pembeni sababu wako slow ukipata mipira ipitishe katikati kwa speed kubwa kama siyo mkude kukuchezea rafu kule nyuma kwa wawa na na onyango unawapita kirahisi sana

halafu wala haina shida kujua formation yao ni 4-2-3-1 kuanzia mwanzo wa msimu hadi mwisho,haijalishi wanacheza na majimaji au tp mazembe,wako nyumbani au ugenini,kishingo keshakariri hivyo maskini ya Mungu anaonekana ni kocha cheap sana ..wtf
Ndo bongo tulivo.. Yan kuwa kocha wa timu za bongo ni kazi kweli kweli..

Hayo ni matokeo tu kama ambavyo mpira ulivyo na matokeo matatu.. Imagine Simba Jana angeshinda sidhan kama Leo ungeandika Uzi wa kocha kutimuliwa.

Yani Simba kila game tushinde tumekuwa nani kwa mfano? Hata wapinzani nao wanakuwa na tactic na lengo la kushinda kikubwa team ijiandae kwa game ijayo..
Hakuna aliyesema tunataka tuwe tunashinda game zote daima, ila pia hakuna shabiki aliye tayari kuona timu inapata matokeo kwa bahati nasibu au kufungwa kizembe zembe.

Hivi umefatilia performance ya Simba kwenye hizi game tatu za mwisho (mbili za VPL na hii ya CL) ? Hii Simba inayowatia pressure mashabiki wake wenyewe wewe unaona iko sawa?
 
Hapo utaona tofauti ya simba na yanga, simba hawana subira ni jazba tu, si watu wa kufanyanha utafiti.

Mtu kama haji manara atawasidia nini mropokaji yule shule hamna.

Ukitaka kumlaumu Kishingo, Anza na MO, na uongozi wote wa simba

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mwanzo wa mwisho wana Simba

Ile peak ya mafanikio kwa kikosi husika ilishapita zamani ikifika pale Simba ilivyotinga robo fainali CAF

BAADA YA pale curve ikaanza kubend

Na Sasa wananchi Ni zamu curve inaaanza kupanda

Kutesa kwa zamu
Ligi bado mbichi.Hata Everton/Tottenham/Southampyon ziliwahi kuongoza kuleee!
 
Hivi wewe ukocha ulisomea wapi?
Nilisomea pale Mpapai wa Mbao Academy.

Kwani unataka kusema nini hapa,kwamba kwakuwa sikusomea ukocha basi sipaswi kukosoa mbinu,mfumo na hulka ya kocha Sven Vandernbroeck?

Mkuu,hiyo ni sawa na kusema sisi Wanatanzania tulikosea kuwakosoa wale Madaktari bingwa wa Muhimbili waliomfanyia upasuaji wa kichwa mgonjwa aliyepaswa kufanyiwa upasuaji wa mguu kwakuwa tu hatujasomea udaktari. Na hata Mahakama iliyoamuru huyo mgonjwa alipwe mamilioni kwa kosa hilo lililofanyoka,baada ya miaka kadhaa kupita, nayo ilifanya makosa kwavile hao Mahakama haina utaalamu wa mambo ya tiba.
 
Hakuna aliyesema tunataka tuwe tunashinda game zote daima, ila pia hakuna shabiki aliye tayari kuona timu inapata matokeo kwa bahati nasibu au kufungwa kizembe zembe.

Hivi umefatilia performance ya Simba kwenye hizi game tatu za mwisho (mbili za VPL na hii ya CL) ? Hii Simba inayowatia pressure mashabiki wake wenyewe wewe unaona iko sawa?

Hakuna aliyesema tunataka tuwe tunashinda game zote daima, ila pia hakuna shabiki aliye tayari kuona timu inapata matokeo kwa bahati nasibu au kufungwa kizembe zembe.

Hivi umefatilia performance ya Simba kwenye hizi game tatu za mwisho (mbili za VPL na hii ya CL) ? Hii Simba inayowatia pressure mashabiki wake wenyewe wewe unaona iko sawa?
Kwa iyo kwa mawazo yako unaona Simba mechi ya juzi na Fc platinum walifungwa kizembe zembe sio?
Kweli wee hupendi mpira unaipenda simba
 
Back
Top Bottom