Heshima kwenu wanasheria. Ninapanga kwenda kupima DNA first born wangu sababu kadri anavyokuwa mkubwa ndo anaonyesha kabisa si mwanangu maana hafanani na mimi wala mama yake, pia hafanani hata na watoto wa kaka zangu, tumezaa mtoto wa 2 wa kike huyu anafanana na watoto wote wa ukoo yaan familia yetu. Na hii huwa ipo hivo watoto wetu wote wanafanana hasa wa kaka zangu na anafanan na mimi kila kitu.
Nimemlea huyu mtoto hadi sasa ana miaka 14. Ninachouliza nawezakwenda kupima DNA bila mama wala mtoto kufahamu
Na kama ikibainika sio wangu najua hakutakuwa na ndoa tena Je, naweza kudai fidia kwa mama yake?
Ikumbukwe mtoto huyu alizaliwa kabla ya kuoana na kila mtu alikuwa mkoa tofauti mm dar yy dom
Kisheri kuna dhana inayosema “kitanda hakizai haramu”
As long as unaishi au unamahusiano na mwanamke na ndani ya ndoa/mahusiano hayo akapatikana mtoto basi itatambulika mtoto ni wako kisheria
Iwapo itatokea issue yoyote itakayopelekea Me kuwa na wasiwasi kuwa ndani ya ndoa/mahusiano Ke alichepuka na kupata mimba kwingine basi kuna taratibu za kisheria zinabidi kufuatwa mahakamani ili kupata kibali kwenda kwa mkemia mkuu wa serikali kupima DNA
Kwa mujibu wa maelezo yako inaonyesha uliikubali mimba na ukamkubali mtoto kama mwanao hadi alipoanza kukua ndio ukaanza kuhisi sio wako(mpaka sasa mtoto ni wako kisheria)
Kama hujaridhika Nenda kaanze mchakato ustawi wa jamii kisha utakwenda mahakamani ambako utapata kibali halali cha kupima DNA wewe na mtoto
Zingatia kwamba upimaji wowote wa DNA ambao hautafuata mlolongo huu basi vipimo hivyo havitatambulika kisheria
Pia unapaswa kujua kwamba serikali ina discourage sana aina hii ya upimaji wa DNA kumlinda mtoto zaidi
So tegemea mlolongo mrefu na mgumu sana kuanzia ustawi wa jamii, mahakamani na kwa mkemia mkuu
Inadaiwa 99.9% ya majibu ya mkemia mkuu kwa issue kama hizi hapa Tz majibu huwa ni mtoto ni wa baba aliyekua na hofu
Mengineyo
Mkuu maisha yalivyo ni kwamba mwanao ni yule aliyezaliwa ndani ya ndoa/mahusiano na ikatengenezwa bond ya mtoto na mzazi
Ukisema tuanze kupimana DNA hii dunia haitakalika mkuu
Binafsi nina watoto wawili nimezaa na wake za watu, tunao jua habari hiyo ni mimi na mama zao tu
Sina muda nao kabisa kwasababu hawanijua wala hawa idea kwamba baba wanao mjua wao sio baba wa kibaiolojia
Wana furaha na “baba” zao na baba hawana wasi wasi
Sina kabisa ujasiri wa kwenda kupima wanangu DNA......... siwezi kufanya huo ujinga abadan
Bond tulionayo mimi na wanangu siwezi kuruhusu mjinga yeyote aikatishe hata kama watoto sio kojo langu
We have a very special bond
LEA “MWANAO” MKUU