Hivi ile kauli ya " Watuhumiwa walitakiwa kutokujibu chochote maana mahakama hii Haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo" imekaa kichuro sana

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Ni kauli ya kushangaza kidogo kama mahakama Haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo Watuhumiwa mmewapeleka hapo kufanya Nini kwanini wasiende moja kwa moja mahakama yenye nguvu kisheria ya kusikiliza kesi za namna hiyo?

Mambo ya zamani Bado tunayashadadia sana Tanzania.
 
Hizi ni baadhi ya sheria za kipuuzi sana, na majaji wetu wanajiona ni wasomi huku bado wanatekeleza sheria zisizo na maana yoyote.
 
Inaonekana wanataka kutii sheria ya mtuhumiwa kufikishwa mahakama ndani ya masaa yaliyotamkwa kisheria.
Sasa unakuta majaji wa hadhi ya mahakama husika hawapo muda huo.
Hii yote umasikini wa serikali kushindwa kuwekeza pesa kwenye mahakama. Mfano kuajiri jaji wa kutosha na kujenga miundombinu ya mahakama ya kutosha.
Ule utaratibu ni uonevu tu na kuvunja haki za watuhumiwa kusikilizwa haraka na mahakama husika.
 
Ni kauli ya kushangaza kidogo kama mahakama Haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo Watuhumiwa mmewapeleka hapo kufanya Nini kwanini wasiende moja kwa moja mahakama yenye nguvu kisheria ya kusikiliza kesi za namna hiyo?

Mambo ya zamani Bado tunayashadadia sana Tanzania.
Hili hata Mimi silielewi!Wakili MSOMI,Halafu mahakamani wapo tuu.
 
Tena gharama za magari,karatasi,kujazana ovyo mahakamani, mwisho wa siku, mahakama haina mamlaka,mnawasomea wa Nini mashtaka kama mmefungwa mdomo na sharia ya kikoloni!?
Hizi sheria za hovyo Wanasheria na Wanaharakati wapo kimya niliwahi kufikiri kuhusu ili swala nikasema ni upuuzi tu hata kama ni sheria ni zile sheria zilizokufa ila bado zinatumika..
 
Back
Top Bottom