Huyu rais Samia anapaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu. Anajua kucheza na akili za watanzania kweli kweli.
Kabla ya kumleta mwarabu alianza kwa kuwaweka sawa wabunge (kama alivyotujuza mbunge wa CDM Aida Kenan). Aliwapeleka Dubai kwa ziara ya "mafunzo". Wakala bata na kupewa cha mfukoni. Suala hili lilipofika bungeni walioenda mafunzoni wakabaki kupiga makofi tu.
Sasa nirudi kwenye mada yangu.
Ili awapoteze kwenye ramani wapinzani, rais Samia akajivika uungwana na akawa anatoa lugha tamu kwao. Akaanzisha kikosi kazi kisichokuwa cha kisheria kujadili, kuchambua na kupendekeza suluhisho. Wapinzani wakaingia likizo, wakalegeza misuli ya mapambano dhidi ya chama tawala.
Mara kidogo akawaita chadema ikulu na kuitangazia nchi kuwa kuna mazuzungumzo ambayo lengo lake ni kujenga maridhiano na utangamano baina ya chama tawala na vyama vya upinzani.
Hii ni hadaa ya karne. Wapinzani walipewa peremende ambayo utamu wake uliwapumbaza na kuwafanya wapoteze dira na mwelekeo wao.
Maana bado miezi tu tuingie kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na bado mwaka na miezi kidogo ili kufika ktk uchaguzi mkuu 2025. Bado kuna ukimya usioelezeka na hakuna kinachofanyika.
Kwa ukimya huu, rais Samia amewashinda wapinzani bila ya kutumia mabavu kama mtangulizi wake (Magufuli ).
Naweza kusema rais Samia ni msanii mzuri sana wa kucheza na akili za wapinzani. Ameshinda vita kubwa na ngumu kwa ulimi tu.