Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Hilo ni swali ninaloliuliza kwa nia njema kabisa.
Ni swali ambalo limekuwa likinijia kichwani mwangu baada ya Rais Samia kuwa Rais.
Nimeona na nimesikia sana kuwa Sasa Rais Samia “ is returning to the authoritarian practices of John Magufuli.”
Hivi, kama Rais akiwa dikteta, wewe makamu wake unakuwa nani sasa?
Unajitengaje na udikteta wa bosi wako?
Kwa sababu, kama wewe makamu hukubaliani na udikteta wa bosi wako, si unajiuzulu tu ili usiendelee kuchafuka.
Sasa unapoendelea kuwa makamu huku matendo ya kidikteta yakiendelea, maana yake ni huoni kibaya kinachoendelea.
Hizi habari za kwamba Rais Samia anarudi kwenye udikteta wa Rais Magufuli, ni bad faith arguments.
Anarudi kivipi ilhali yeye ndo alikuwa makamu wa Rais wa Magufuli?
Dkt. Mpango yeye hahusiki kabisa na chichote ambacho bosi wake, Rais Samia, anachokifanya?
Kama Magufuli alikuwa ni dikteta basi Samia harudi kwenye udikteta. Ni mwendelezo wa matendo ya timu ile ile iliyokuwepo.
Tofauti iliyopo sasa ni kwamba aliyekuwa kocha msaidizi ndo kawa kocha mkuu.
Watu waache kujitoa ufahamu.