Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Wizi, uongo, ulaghai, kuumiza wengine huo ndio uchawi wenyewe..., hayo mengine labda kama unataka kuwa mtaji wa matapeli
 
Mkuu ni Mungu anakupenda sana ila uchawi upo sema usiuendekeze sasa.
Wengi huwa wanauendekeza kitu kidogo nimerogwa.
Ila uchawi kuwepo upo mkuu.
Tena wazungu na waarabu ndio wachawi wakuu duniani.
 
Hamna kitu kinaitwa uchawi duniani labda mazingahombwe
Kwahiyo mkuu hawa wanaoenda kwa waganga ili kumroga mtu kumtia stroke, uchizi au kumuuwa kabisa huwa inakuaje sasa ni kwamba hakuna kinachotokea au mganga anafanya mazingaombwe gani?
 
Laiti uchawi ungekuwepo Lissu asingekua gerezani saa hizi dearest.
 
Hapo umethibitisha kwamba hakuna uchawi duniani au hakuna uchawi wa chuma ulete au umethibitisha huyo mbaba sio chuma ulete?
 
Wachawi walikuwepo zamani wakiongozwa na Mshana Jr . Ila sasa amegeukia upande wa pili anajiandaa kuwa mchungaji uzeeni
 
Kwahiyo mkuu hawa wanaoenda kwa waganga ili kumroga mtu kumtia stroke, uchizi au kumuuwa kabisa huwa inakuaje sasa ni kwamba hakuna kinachotokea au mganga anafanya mazingaombwe gani?
Unaweza thibitisha kuwa mtu kauliwa na uchawi au kapewa stroke?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…