Hivi ina maana wachawi hawapo kabisa JF?

Mimi naishi Simiyu na nasema uchawi haupo!

Period, end of it.
 
Huo ni uzuzu wa mwenye kuamini hayo maujinga sio uchawi. Kwani nikuulize

Bila uchawi hakuna uchizi?

Bila uchawi hakuna kifo?

Nijibu ili nikuelimishe
 
unahitaji ushahidi upi mkuu?

ungehitaji picha au video ya kitu kinachoitwa uchawi?
Tunathibitisha vitu kupitia

1. Senses k.v kuona, kusikia, kunusa au kuhisi
2. Vipimo vya kisayansi k.v thermometer (joto), Barometer (mgandamizo wa hewa)

Thibitisha au muite huyo mkuu wa wilaya athibitishe kiwepo kwa uchawi hilo eneo uliosema
 
Sidhani sidhani zako ni nyingi mno.

Unawezaje kuthibitisha kuwa uchawi upo?
Wewe si ndio unasema hakuna uchawi na kama upo basi mtu akuroge? Sasa tena mbona unaniuliza mie kama naweza kuthibitisha kama uchawi upo?

Mimi nataka wewe unaetaka kurogwa ndio ueleze kurogwa kukoje maana isije ukawa unasema hakuna aliyeweza kukuroga na unahitimisha hakuna uchawi wakati haujui huko kurogwa kwenye kukoje.
 
atoe tu evidence --- ila hapo ndo mzozo ulipo
Nitoe evidence ya nini? Mbona mnakuwa watu wa kukariri? Nyie mnaleta madai hapa ila hayo madai yenu yakihojiwa mnageuza kibao mnakimbilie kudai evidence.
 
Pale tabora kuna jamaa aliitwa mwana wa nshimba manywele...

Huyu bwana alikua mwindaji...

Alikua akiingia polini kuwinda twiga au nyati alikua haonekani na askari wanyama poli...

Ukiacha huyo, kuna mzee alikua anawinda tembo...

Alikua akifika kwenye kundi la tembo anapima kwanza zile pembe kwa mkono...

Akipata mwenye pembe anazotaka anaanza kuwapiga risasi tembo wamezubaa hadi amalize ndio wanashituka kukimbia...

Nyinyi msioamini uchawi, hiki kitu mnakiitaje kitaalamu?
 
oya man hakuna kitu inaitwaga uchawi ni fiction tu izo bob we unadhani uchawi ungekuwepo watu wangekuwa wanateseka kiasi hiki? ni suala tuu lakutumia uchawi kazi inaisha chap
Mbona hata Mungu ameshindwa kumaliza watu kuteseka duniani
 
Story za abunuasi ukiambiwa ulete ushahidi wa hayo matukio uliotaja utaanza kuruka ruka
 
Kusikia watu wakisema au kusikia mlio wa kichawi?
Una uhakika gani alikuwa haonekani na walinzi wa misitu?

Una uhakika gani kuwa alikuwa akiwashika tembo mapembe kabla ya kuwaua?

Unaamini story za uwongo leta ushahidi wa story yako
 
Mbona hamjawahi jitokeza kutupa Elimu,mlianzaje,mkakomaaje,mnafanyaje na mnafaidikaje au mnababukaje na maombi ya watu wenye Imani ya kweli?

Nimeona mpo kimya sana au ndiyo kujisahaulisha tu?
Ngoja waje,napenda kuwasikia na kuwaona live!! Hivi wakoje? ,pia waje watwambie wanafaidikaje kwa kwenda kilometa kadhaa,,kwa ajili tu yakumpiga mtu chale?!!
 
Hoja zao za kitoto kichizi, mtu anakwambia kama uchawi upo mbona hawaibi bank wakati huo anakataa kesi za uchawi wa chuma ulete huku mitaani na sababu ya kukataa ni kwamba hakuna uthibitisho, sasa najiuliza hata akiambiwa watu wameiba kichawi bank bado hatokubali atasema hakuna uthibitisho. Mwengine anataka arogwe kama kweli uchawi upo wakati huo hata hajui huko kurogwa kukoje ili aweze kutofautisha kurogwa na kutokurogwa kama anangojea aote mkia ndio ajue karogwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…