covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,355
- 20,792
Hivi inawezekanaje mtu mmoja kama Rostam kuweza kuwapita akili na ku-outsmart viongozi wetu wakubwa, wanasiasa, wakurugenzi, mameneja wa mashirika makubwa ya umma na hata vyombo vya ulinzi na usalama? Swali hili linaacha mshangao mkubwa.
Je, ni kwa sababu yeye ni genius, au kuna udhaifu mkubwa kwenye mifumo yetu?
Tumeona mara nyingi kwa sasa Polepole akimlenga Rostam kama chanzo cha ufisadi wa muda mrefu nchini. Ameeleza kwa undani jinsi jina lake linavyohusishwa na vigogo wakubwa serikalini, na kwa namna ya kushangaza, historia hii inarudi nyuma tangu mwaka 2005 hadi leo. Rostam ni tycoon, mtu mwenye nguvu kubwa kwenye anga za uchumi na siasa, na ukiunganisha nukta za maelezo ya Polepole, unaweza kuona kuna ukweli kwa kiwango kikubwa.
Lakini maswali amaboyo najiuliza:
Huyu mtu anapata wapi muda wa kufanya “deals” zote hizi kubwa zinazohusisha mabilioni ya fedha? Amewezaje mara kwa mara kuwapiga chenga marais na mawaziri wetu? Na zile pesa zote nyingi ambazo amekuwa akizipata kwa miaka yote hii zinakwenda wapi? Je, ni kweli anapiga hela hizi kwa faida binafsi tu, au kuna mtandao mkubwa zaidi unaofaidika nyuma yake je huu mtandao unatoka nchi gani hasa?
Cha kushangaza zaidi, kuhusu maisha yake binafsi hatuna taarifa nyingi. Hata familia yake haijulikani waziwazi, hujawahi kusikia habari za mke au watoto wake. Ni kana kwamba maisha yake binafsi yamefunikwa kwa makusudi ili kuendelea kumfanya aonekane ni mtu “untouchable”.
Na pia, kwa nini kila awamu jina ni lilelile? Kwa nini mara zote ni Rostam? Wapo mabilionea wengine wakubwa kama Mo Dewji, Bakheresa na wengine ambao hawajawahi kutajwa mara kwa mara kwenye skendo kubwa za kisiasa na kiuchumi. Kwa nini ni yeye peke yake anayejitokeza kila mara?
Mwisho wa yote, swali langu kubwa lipo kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama:
Hivi mnashindwa vipi kudhibiti mtu mmoja anayeonekana kila mara kuwavuruga viongozi wetu wakuu? Inakuwaje mtu mmoja anachafua taswira ya viongozi, hadi hata pale ambapo kiongozi mpya akiingia madarakani kwa matumaini na mapenzi ya wananchi, baada ya muda mfupi taswira yake inaharibika kwa sababu ya kushirikiana au kuhusishwa na huyu bwana?
Wananchi wa kawaida, ambao hatuna ushabiki wa kisiasa, tunabaki na maswali mazito. Vyombo vya ulinzi na usalama mnafanya kazi kwa maslahi ya nani? Ni kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla, au kwa maslahi ya mtu mmoja na mtandao wake? Kwa sasa, badala ya kuwa kimbilio la usalama na amani, vyombo hivi vimeanza kuonekana kama sehemu ya kuongeza taharuki.
Hii inaleta hofu kubwa kwa mustakabali wa nchi na vizazi vijavyo.