econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Najiuliza swali kubwa Sana. Hivi inteligensia ya Polisi wa Tanzania ni Kwa CHADEMA tu?. Yani CHADEMA ndio pekee wanaomulikwa na polisi?
Binti anabakwa na vijana Sita na polisi hawajui mpaka Video ilipowekwa hadharani ndipo wakaanza kuhaha ila mpaka Leo hakuna hatua iliyochukuliwa. Nikawa najiuliza Kama Jambo baya Kama Hilo linafanyika na polisi hawajui, je inteligensia yao ni kubwa kiasi gani?. Cha kushangaza polisi wasiokuwa na intelejensia kwenye makosa ya jinai, wanakuwa wepesi kuwa na intelejensia kwenye siasa hasa Kwa chama Cha CHADEMA.
Kwenye Ziara ya Makonda kipindi akiwa mwenezi wa CCM ilionekana wazi polisi wamezidiwa na kupotea Kwa watu. Watu wanatekwa na watu wasiojulikana na kupotelea kusikojulikana na polisi wapo kimya. TLS wameitoa orodha ya watu waliopotea mpaka Leo wanaokaribia 80 ila Polisi wapo kimya Kama hawajui chochote.
Polisi hawajui nani alimshambulia Lissu, polisi hawajui Ben Sanane alipotelea wapi na polisi hawajui Azory Gwanda alipotelea wapi?. Yani itelijensia yao imefikia kikomo. Lakini inteligensia yao ipo juu linapofika suala la CHADEMA ndio utaona unafiki wao.
Polisi badilikeni acheni ujinga.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Hivi hili swali la Oscar Oscar kati ya CCM na jeshi la Polisi nani wanaotakiwa walijibu?