Hivi itanigharimu kiasi gani nikitaka kufungua studio ndogo ya kurekodi Muziki?

Hivi itanigharimu kiasi gani nikitaka kufungua studio ndogo ya kurekodi Muziki?

nina kinanda yamaha psr 9000 anayejua jinsi ya kurekodi beat au nyimbo anielekeze tafadhali. yani hki kinahtaji mtu ajue mana kina maneno mengi.
 
Studio ya mziki ukiwa na milion 5 unasuka studio kali sana.. studio ya mziki sio gharama kabisa hata milion 3 inatosha kanaoweza

Studio ya mziki ukiwa na milion 5 unasuka studio kali sana.. studio ya mziki sio gharama kabisa hata milion 3 inatosha kusuka studio
Mimi tayari nimeshanunua vifaa sasa natafuta eatu watao weza kunifungia soundroom ndogo tu ili niweze kuanza kazi.....naomba msaada chief
 
Kwa makadirio ni kama ifuatavyo:
1. Pc yenye uwezo kwa bei za kariakoo ni 2m
2. Monitor speakers za yamaha (hs 8) ni 2.4m na mkononi ni 1.8m
3. Sound card /audio interface ya njia mbili ndani na nne nje ni laki saba hadi tisa kulingana na brand kama focusrite, avid, m audio, presonus, behringer na kadhalika.
4. Microphone: kwa hapa dar nisikudanganye tu mkuu ukienda kariakoo utakuta hizi mic za mchina kama turkstar zimejaa kuanzia laki tatu ila sikushauri ununue. Mic nzuri ni ile ambayo bei zake zipo kuanzia laki nane au uipate kutoka kwa mtu. Kama utapata audio technica at 2020 itafaa sana na kuna siku niliwahi kuiona huko kariakoo duka la congo music shop
5. Midi keyboard controller huanzia laki tano na nusu kulingana na aina ya midi controller unayoitaka, kuna za keys 49, 61 hadi 88 na pia huwa zinakuwa semi weighted au full velocity.
6. Software kwa ajili ya productions pamoja na audio samples. Hizi ndio silaha za maangamizi kwenye production na sio rahisi sana kuzipata. Huwa mtu anakufanyia installation kwa package ya laki tatu kwa plugin za kawaida au laki 8 kwa full package ya world class samplers, synthesizers na plugins za mixing na Mastering.
7. Cables, stands na accessories: hizi mara nyingi huwa bei rahisi na huweza kufika laki sita kulingana na quality yake.
8. DIY Acoustics treatment: hii mara nyingi hutegemea na aina ya chumba utakachofanya kuwa studio na mimi binafsi nashauri uwekeze kwenye zile movable panels ambazo ukutaka kuhama ni rahisi kuzitoa na gharama zake ni approximately laki sita kwa chumba cha wastani.
9. Furniture: utahitaji kiti na meza kwa ajili ya prodicer, sofa set kwa ajili ya wageni na wateja na carpet
10. Air conditioner; kwa kawaida unahitaji a/c ya 9,000 btu/hr au 12,000 btu/hr kama chumba kitakuwa kikubwa kiasi
nawapataje hawa watu wa kunifungia hizi Diy acoustic treatment mkuu...mimi swala la vifaanimesha malizana nalo
 
IMG_20220909_133325_859.jpg
nina midi hiyo 49keys 300,000 tu
 
Mkuu nitakupinga baadhi ya mambo hapo, ila ni katika kujaribu kupeana elimu ya mambo ya utayarishaji wa muziki,
Studio ndogo ya kurekodi muziki huhitaji mixer kwa sababu sauti hutumia conversion ya sound card.

Na pia suala la monitor speakers sio kwa bei hiyo unayosema kwa sababu uwezo wa monitor ndio utaamua output ya muziki wako, kwa mfano ukitumia hizi m audio hutapata output nzuri kama anyetumia yamaha au krk rokit.

Pia uwezo wa computer katika kuhimili vst/au/aax plug in ni kipaumbele namba moja. Hivyo fedha kubwa itumike kwa vipaumbele vifuatavyo:

1.monitor speakers
2.computer pamoja na software plugins zake
3.Mic na audio interface
4. acoustic treatment
5.vinginevyo
Ndio uweke na bei maana jamaa kamtajia vya bei ya sawa na bure
 
Back
Top Bottom