mfanyabiashara mashuhuri jack pemba akiwa na wachezaji nyota wa zamani wa uingereza alipowaleta mwaka jana bongo. habari za uhakika zinasema mgogoro ulioumuka katika kampuni ya kusaka na kukuza vipaji ya global scouting bureau (gsb) umekwisha na yeye ameonekana hana tatizo na kupewa shavu la kuendelea na kazi yake ya umakamu wa rais katika shughuli za kimataifa. pia habari zimeeleza kwa sasa yeye amenunua hisa kwenye gsb na kuwa mkurugenzi na sio mwajiriwa tena.
katika mahojiano yangu kwa njia ya simu na rais wa gsb, james gamble, alieko marekani, amenithibitishia hayo na kuongeza kwamba jack pemba hakuwa amefukuzwa gsb bali amesimamishwa ili kupisha uchunguzi ufanyike kuhusu mambo kadhaa ikiwemo ubadhiulifu wa pesa na kwamba amekutwa hana hatia na amerejea kazini kama kawaida. jack pemba pia nilipoongea nae kathibitisha hilo na kusema anatarajiwa kurejea bongo hivi karibuni kuendeleza libeneke pale alipokomea baada ya mgogoro kuumuka.
SOURCE:
http://issamichuzi.blogspot.com/