Hivi jamani ni haki kweli Kwa wanafunzi wa darasa la nne msingi kusoma mpaka saa tatu usiku na shule ni ya day....?

Hivi jamani ni haki kweli Kwa wanafunzi wa darasa la nne msingi kusoma mpaka saa tatu usiku na shule ni ya day....?

kadeti

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
1,115
Reaction score
1,105
Kuna shule moja ipo mwanza ambako mwanangu anasomea, nimeshangazwa na taharifa ya Mwalimu Mkuu wa iyo shule akiwataka Wazazi kuanza kuwaijia watoto wao shule.

Hii imetokana na kubadilika Kwa ratiba za masomo Kwa wanafunzi kwamba wanapaswa kusoma mpaka muda wa saa tatu usiku kuendana na maandalizi ya mitihani yao.

Kwakweli sikukubaliana na iyo hoja kwani ilinivurugia ratiba yangu ya maisha Kwa ujumla.

Na nikajiuliza hayo masomo ambayo mtoto wa darasa la nne anasoma ni magumu kiasi gani Cha kuitaji msuli mkubwa hivyo.

Kiasi kwamba mtoto anapotoka Shule hawezi Fanya lolote nyumbani hata homework zake..anaishia kulala tu na kachoka ballaha.

Sasa najiuliza hizi taratibu za shule za day kusoma mpaka saa tatu usiku mamlaka wanajua au mpaka paje patokee majanga ya kimaadili au watoto kufanyiwa vitendo viovu nyakati hizo za usiku...!
 
Nadhani ilipaswa iwe ni hiari ya mzazi na mwanae, binafsi hata shule anayosoma mwanangu wanayo hiyo ratiba Kwa yule mzazi atakaeona inampendeza! Mwanangu aliijaribu kama wiki akawa dhoofu la hali, maana ilimlazimu kuamka saa 11 asbh na kurudi saa 4 usiku...nikasema hapana na ikawa hivyo...ni ratiba ngumu Kwa mtoto na haitekelezeki...ilifikia mahala mtoto akaanza kuhoji, alisema mwl katwambia tulale masaa yasiopungua 8, je mbona mm nalala masaa chini ya 8?
 
Serikali iingilie hizi ratiba za EMS aisee, ni mbaya.

Mdogo wangu yupo la kwanza lakini anatoka shule saa 12 jioni...
 
mwanangu yuko chekechea wanamtoa saa 12 jion, nikasema no,,

sasa kanatoka saa 6 mchana 👍
 
Taharifa=Taarifa
Iyo=Hiyo
Ballaha=Balaa
Kuitaji=Kuhitaji
Kuwaijia=Kuwajia,,,,Acha Mtoto Asome Unataka Afuate Nyayo Zako
Ndio anasoma ila sio mpaka usiku wote huo, yaan kurekebisha hizo herufi ndio mpaka saa tatu za usiku?
 
Unaweza kufikiri Mwalimu anapigania ufaulu na maendeleo ya mwanao.
BIG NO.
Hapo anapigana alama na ufaulu wa juu kwa manufaa yake na hajali chochote kuhusu mwanao.
Ova.
 
Sijui ni uelewa mdogo wa walimu ama ni kujifanya wapumbavu tu, ubongo wa binadamu achilia mbali mtoto mdogo una limit ya kuweza concentrate kwa siku moja.

Akili ikichoka hata ufundishe nini hakiingii kichwani kwahiyo kiuhalisia ni sawa na kupoteza muda kumuweka mtoto shule kwa masaa mengi kwa matarajio ya kuelewa zaidi.

Enzi tulizosoma sisi (90's-2000's) kulikuwa hakuna mambo ya kuwekana madarasani mpaka usiku wa manane na bado watoto walisoma na kuelewa na matokeo mazuri kupatikana.

Mashule mengi kwa sasa yanajali vipato vyao kuliko afya ya akili ya mtoto. Nina hakika kwa hayo masaa ya ziada watataka ujira zaidi. Hivyo ni faida kwao.

Kijana wangu alipokuwa darasa la saba mwaka 2023, shule ilileta barua kuwa ni lazima ahamie boarding kwa maandalizi zaidi. Na kuwa inapaswa nilipe ada ya karibia 350,000 kila term.
Nilikataa na kuwaambia ninaishi takriban dakika 5 kutoka shule ilipo hivyo wakimuhataji saa yeyote waniambie nitampeleka. Mwisho wa siku kulikuwa hakuna lolote la ziada walilokuwa wanafundishwa zaidi ya prep wanayojisomea wenyewe.
 
Hope likud hajapata point ya kugandamizia hapa. Ni Ems au st kayumba?
 
Mtoe mwanao (pekee)kwenye masomo hayo ya ziada sw.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Unaweza kufikiri Mwalimu anapigania ufaulu na maendeleo ya mwanao.
BIG NO.
Hapo anapigana alama na ufaulu wa juu kwa manufaa yake na hajali chochote kuhusu mwanao.
Ova.
Ukweli mtupu na mbaya zaidi wazazi wengi hawalioni hili

Watoto wanageuzwa mitaji na misukule ya shule. Mmiliki wa shule anajua kabisa mtaji mkubwa kwake ni kufaulisha hivyo ataburuza hao watoto hadi atimize malengo yake

Imagine mtoto anatoka nyumbani 12 asubuhi kurudi ni saa 3 usiku, hata wafanyakazi wa viwanda vya wahindi hawana hii ratiba.
 
Back
Top Bottom