Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni haki ya msingi Kwa chama chochote Cha siasa kufanya maandamano ya amani Ili kufikisha ujumbe muhimu Kwa serikali inayotuongoza.
Hata hivyo haki hiyo imekuwa ikiminywa na watawala Kwa kulitumia Jeshi la Polisi, Kwa kisingizio tu Cha taarifa walizonazo za kiintelejensia Kwa kukataza haki hiyo ya kikatiba.
Tukumbuke kuwa CHADEMA waliitisha maandamano yao amani tarehe 23 mwezi huu, wakisema kuwa watakuwa wanaomboleza kifo Cha kiongozi wao mjumbe wa sekratarieti wa chama hiko, Ali Kibao, ambaye aliuawa kinyama na mwili wake kutupwa huko Ununio na vile vile kuishinikiza serikali hii ituambie wako wapi viongozi wa CHADEMA, akina Soka, ambao walitekwa zaidi ya mwezi hivi sasa na hawajulikani waliko.
Ndipo Jeshi la Polisi likatia hiyo taarifa yao kuwa eti wameyapiga marufuku maandamano hayo Kwa kisingizio tu Cha taarifa walizonazo nazo ni kuwa maandamano hayo Yana viashiria vya uvunjifu wa amani!
Ni kawaida sana Kwa kipindi Cha sasa Kwa Jeshi hili la Polisi kuminya uhuru wa kufanya siasa Kwa chama Cha CHADEMA.
Kwa kuwa Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufanya maandamano ya amani ni ruksa na kinachotakiwa na Jeshi la Polisi ni kuyapa ulinzi maandamano hayo Ili usiwepo huo uvunjifu wa amani "unaotabiriwa" kutokea katika maandamano hayo.
Hebu tujiulize katika kuyavunja maandamano hayo ya amani ya Chama Cha CHADEMA wiki iliyopita, Kwa kuleta vikosi vya Jeshi la Polisi vya nchi nzima, yalitumika mapesa mabilioni mangapi, ambazo ni pesa zetu walipa Kodi wa nchi hii??
Hebu pia tujiulize iwapo kweli Jeshi letu la Polisi ni mabingwa wa kunusa intelelejinsia kama wanavyodai wao wenyewe, ni kitu Gani kilichowafanya washindwe kung'amua intelelejinsia kuwa Mbowe hayupo nyumbani kwake Mikocheni, badala yake wakaweka ulinzi wa saa 24, Kwa siku 3 mfululizo Ili wamzuie Mbowe asihudhurie maandamano hayo, badala yake Mbowe aliibuka Kwenye maandano hayo ya amani siku ya maandamano hayo Magomeni Mapipa?
Soma Pia: Maandamano ya CHADEMA: Mbona Jeshi la Polisi halijajibu maswali ya msingi waliiyoulizwa na CHADEMA, badala yake wanaendeleza vitisho vyao?
Badala ya kupoteza mabilioni ya mapesa ya walipa Kodi wa nchi hii, ni vyema Jeshi letu la Polisi, likauzingatia ushauri muhimu sana alioutoa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, mwaka 2012 katika kikao Cha mkutano Mkuu wa CCM, alipowaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa CCM isipende kulitumia Jeshi la Polisi kuwapendelea wao, bali hoja za upinzani zijibiwe Kwa hoja Kwenye majukwaa ya kisiasa, badala ya kulitumia Jeshi la Polisi na mitutu yao ndiyo walitegemee walijibie Kwa niaba yao hoja zao za kisiasa na akaendelea "kukitabiria" chama hicho kuwa utafika wakati Jeshi hilo litagoma kupokea tena maagizo ya Chama Tawala na watawaeleza wanaccm kuwa wao watatekeleza majukumu yao Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Wala siyo Kwa nia ya kukipendelea chama hicho Cha siasa.
Mungu ibariki Tanzania