Hivi jeshi wanaruhusu kupokea mtu mwenye miaka 29/30?

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Mambo yanakwendaje wadau kwa mtu ambae tiyari ni degree holder na ana passion ya kwenda jeshi ni umri gani wa juu wa mwisho jeshi Lina chukua recruit!

Na kama huna cheti cha Jkt je mafunzo ya Jwtz? Unaweza ruhusiwa kujiunga?
 
Kwa ngazi ya degree kisheria mwisho huwa ni 30, lakini ukiwa na connection hata 35 unazama.. and yes bila cheti cha jkt unaweza zama kama una mtu mzito nyuma yako.
 
Sio mbaya imekaa vizuri
 
Mambo yanakwendaje wadau kwa mtu ambae tiyari ni degree holder na ana passion ya kwenda jeshi ni umri gani wa juu wa mwisho jeshi Lina chukua recruit!

Na kama huna cheti cha Jkt je mafunzo ya Jwtz? Unaweza ruhusiwa kujiunga?
Infact,
kati ya 2012-2014 waliajiriwa jeshini professionals wenye hadi wenye over 30 years and below 45 years.
Hiyo ni kumaanisha, pakiwa na uhitaji huo kwa wakati muafaka 🐒
 
Kwaida ila vigezo huwa inakua kwenye Elimu, huwezi kuwa darasa la saba alafu wakuajiri na miaka 30
 
Sio tu kuingia huko unaweza kupata hata Kazi bila kwenda depo.

Kuna kijana Aliingiziwa jeshi moja na hakwenda depo yoyote so inawezekana kabisa.
Haiwezekani mzee usipo pitia depo we mwenyewe hiyo kazi hautaweza kufanya
 
Tafuta mtu akushike kama upo mtaani tena awe mzito na pia awe mnjanja anajua chocho za kupita unaingia
 
Kama kuna mtu Ana nyota moja anaweza kumpigia pande akaingia huko ?

Yupo mtu ni mshikaji wangu Ila sijawahi kumuuliza hizo habari nawaza njia ya kumsaidia kijana kupitia influence yangu.
 
Kuna daktari bingwa pale mount Meru Arusha aliombwa Sana kujiunga kua daktari wa jeshi pale monduli kipindi kile wamejenga hospital Yao ya jeshi, huyu daktari alikua in 40's huko.....

Sema kupiga mwaka mmoja depo la kuvuliwa uraia lazima mkuu(japo walipewa maelekezo amalize tu)

Walivyomaliza, kipindi hiko kikwete ndo alikua rais, kwenye kupewa vyeo jamaa walivyoitwa watu wa nyota Moja yumo, ikaja zamu ya nyota 2 yumo, ya u captain yumo, akaja kumalizia kupewa bibi na bwana kabisa( meja)......

Ukiwa na elimu na jeshi linakuhitaji unaingia bila shida kabisa....

Ila bila elimu nadhani 25 hapo ndo mwisho kama sikosei
 
Kama kuna mtu Ana nyota moja anaweza kumpigia pande akaingia huko ?

Yupo mtu ni mshikaji wangu Ila sijawahi kumuuliza hizo habari nawaza njia ya kumsaidia kijana kupitia influence yangu.
Kua makini sekta ya kuingiza watu jeshini Ina matapeli wengi Sana,
 
Kama kuna mtu Ana nyota moja anaweza kumpigia pande akaingia huko ?

Yupo mtu ni mshikaji wangu Ila sijawahi kumuuliza hizo habari nawaza njia ya kumsaidia kijana kupitia influence yangu.
Uwezo anao ila awe mjanja sana kumbuka huyo anatoka mtaani sio jkt ila uwezo anao ishu nikuongea tu
 
Yeye yupo Kwa wale jamaa wa karoti nadhani ushawajua .!

So nawaza kuongea nae ili wakitoa nafasi nimuombee huyu mdau mwenye age 30.
 
Haiwezekani mzee usipo pitia depo we mwenyewe hiyo kazi hautaweza kufanya
Ni kweli kuwa askari ni mafunzo kijeshi huwezi kupata title ya uaskari kama hujapitia depo
 
Back
Top Bottom