Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Katika utengenezaji wa mbolea kitu kigumu kupata ni Phosphate. Hii haiwezi tengenezwa kama material zingine za mbolea, Nitrates nk. Phosphate huchimbwa. Duniani nchi inayoongoza kwa kuwa na phosphate nyingi ni Morocco. 75% ya phophate yote duniani ipo Moroco. Tani bilioni 50.
Mazao yanapokua, yanaondoka na phosphate(Phosphorous) ardhini. Ardhi inachoka na kuishiwa rutuba.
Lakini Mungu hajatutupa na sisi. Tanzania tuna Phosphate Minjingu ya tani milioni 10. Ipo Mbeya karibu na uwanja wa Songwe, tani zaidi ya milioni 300. Na nyingine ipo huko mkoa wa Songwe.
Kwa nchi inayotegemea kilimo, kuna kitu muhimu kuliko kuzalisha mbolea? Kazi inayotakiwa ni kuichimba na kuiprocess ifae kwa mbolea. Hatuwezi kufanys hii kazi? Huko Morocco serikali ndiyo inamiliki mgodi/migodi ya phosphate, ni jambo nyeti.
Kama nchi tuache kelele za bei ya kuagiza mbolea, nani kaagiza nk nk. Tuzalishe mbolea hapa nchini. Serikali ihakikishe mbolea inazalishwa kwa ufanisi.