GE2025 Hivi Kamanda Muliro anadhani Uchaguzi ni kutangaza tarehe na kugawa maboksi tu?

GE2025 Hivi Kamanda Muliro anadhani Uchaguzi ni kutangaza tarehe na kugawa maboksi tu?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Yaani ukiona Polisi wanatumika kisiasa ogopa aisee .Wanamdanganya Raisi Samia mpaka raha wakitoka hapo wanamx'ong'y .Samia nakushauri tu kama Mama mtanzania kaa macho wamekuzunguka wanakuimbia mapambio huko rohoni hawako na wewe.Nakupenda my dear ,ila kura sipigi mimi na nyumba yangu.
Mama Hana hata presha maana rimoti ipo msoga palee inafanya yt yanayoendelea ktk taifaa😀😀
 
CCM na vyombo vya dora vina maigizo 🤣🤣🤣

Haya sasa, Kamanda Muliro yupo live anatufundisha Katiba ya CCM badala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Eti CHADEMA kuzuia uchaguzi ni kinyume cha Katiba, lakini kuvunja Katiba kwa kuficha Daftari la Wapiga Kura, kutoanzisha Tume Huru, na kupitisha matokeo ya wizi ni uzalendo wa hali ya juu! 😂

Hebu tuwaambie ukweli kwa kejeli safi:

Hivi Kamanda Muliro anadhani uchaguzi ni kutangaza tarehe na kugawa maboksi tu? Wabunge wa CCM walivyokula kiapo cha kuwavua wanasiasa wa upinzani majimbo yao kwa nguvu ya polisi na msajili, hiyo ilikuwa katiba ya nchi gani? 🤣

Wanatetea uchaguzi wa wizi kwa kisingizio cha “Katiba” lakini kwenye uchaguzi wa chama chao ni marufuku kuomba nafasi ya kugombea Rais, mgombea ni mmoja tu — anapita bila kupingwa na wanaita hiyo ni “utamaduni wa CCM.” 😂

CHADEMA hawasemi wanazuia uchaguzi — wanasema “Hakuna uchaguzi bila haki.” Wanataka uchaguzi wa ukweli, sio filamu ya CCM na polisi wake wakiwa waamuzi, mabeki, na washambuliaji.

Kwa kifupi Kamanda Muliro anaongea kama mtu anayejua kalenda ya uchaguzi lakini hasomi ramani ya haki. 😂

Kama mtu akikuita kwenye mbio huku akiwa na bunduki na anasema “shindana bila kuogopa,” lazima umuulize: “hii ni mbio ya haki au mbio ya kuua?”

Chadema wanasema:



Kamanda Muliro anasema:



Kwa hali hii, ni heri CHADEMA wavae suti za heshima za kutokushiriki, kuliko kuvaa mavazi ya harusi ya uchaguzi wa wizi unaoongozwa na serikali yenye njaa ya madaraka.
Na waione Muliro na genge lake la utekaji
 
Yeye kazungumzia suala linalomuhusu ikiwa ni pamoja na kusimamia katiba kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na lazima awaonye wanaotaka kuleta vurugu maana yeye ndo first responder ikitokea vurugu.

Suala la jina lako hulioni kwenye daftari sijui tume huru ya uchaguzi siyo kazi yake , ukitaka kujua kazi yake we nenda kafanye fujo siku ya uchaguzi
Muliro ana elimu gani?
Muda wake wa kustaafu ni lini?
 
Yeye kazungumzia suala linalomuhusu ikiwa ni pamoja na kusimamia katiba kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na lazima awaonye wanaotaka kuleta vurugu maana yeye ndo first responder ikitokea vurugu.

Suala la jina lako hulioni kwenye daftari sijui tume huru ya uchaguzi siyo kazi yake , ukitaka kujua kazi yake we nenda kafanye fujo siku ya uchaguzi
Na mabox kura fake kuingizwa na polisi kwenye vituo vya kura nalo ni la nani?
 
Yeye kazungumzia suala linalomuhusu ikiwa ni pamoja na kusimamia katiba kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na lazima awaonye wanaotaka kuleta vurugu maana yeye ndo first responder ikitokea vurugu.

Suala la jina lako hulioni kwenye daftari sijui tume huru ya uchaguzi siyo kazi yake , ukitaka kujua kazi yake we nenda kafanye fujo siku ya uchaguzi
Murilo ni msemaji wa serikali? Mambo ya reforms ni mambo sio askalli kutoka uko kuja kusema mambo ya vyama uoni kama Murilo kuongelea mambo ya reforms ni kuwapa wale kibali wale wanaosema police ushirikiana na chawa tawala kuiba kura yeye mambo ya reforms hayamuhusu Je reforms zikifanyika hataweka wapi sura yake
 
Back
Top Bottom