Wabunge kuzungumzia bungeni matatizo ya wananchi wanaowaongoza ktk majimbo ni kitu kingine, na serikali kuyapa umuhimu unaostahili matatizo hayo na kutenga fedha kwa ajili ya kuyatatua ni jambo lingine kabisa. Licha ya bunge mubashara kuwekwa kapuni, lkn wabunge karibu wote wakipata fursa ya kuchangia mijadala mbalimbali huwa wanaelezea kero mbalimbali zinazowakabili wapiga kura zao.
Tatizo ni uwezo wa kifedha wa serikali ktk kuweza kuyatatua yote kwa pamoja. Bajeti ya serikali tu inatenga kiasi kidogo sana katika shughuli za maendeleo ili kwa kiasi kikubwa zitumike ktk shughuli za kijamii. Badala yake sehemu kubwa ya fedha zinazotengwa ni kulipia shughuli za uendeshaji wa mambo ya serikali.
Serikali iangalie uwekano wa kufuta baadhi ya vyeo visivyo na tija mikoani na wilayani ili kupunguza gharama za uendeshaji. Mathalani, sidhani kama vyeo kama cha DC na RAS na watendaji waliokuwa chini yao wanahitajika. Ilipasa RC awe na maDAS tu chini yake ambao wanawajibika kwake moja kwa moja ktk masuala ya kiutawala wilayani.
Hapo bado hatujagusa taasisi na wakala wengine wa serikali ambao shughuli zao zinashabihiana sana, ambazo zinaweza kuratibiwa na "single authority". Kwa hiyo basi uwezo wa serikali ktk kutatua kero nyingine utaongezeka endapo serikali itafanya "down sizing" ili iweze kuwa na watendaji wachache tu wenye kuweza kuendesha shughuli zake kwa tija na gharama nafuu.
Serikali iipe umuhimu wa kipekee sekta binafsi, na hata ktk miradi mikubwa ya uwekezaji ifanyike kupitia PPP. Serikali isimamie utekelezaji mzuri wa sera na kutunga sheria rafiki zenye kuchochea maendeleo ya wananchi na siyo hizi za sasa za kichoyo zenye kulinda maslahi ya watawala.