Hivi kampuni za kukopesha mikopo mtandaoni zinamilikiwa na nani? Mbona hazichukuliwi hatua?

Hivi kampuni za kukopesha mikopo mtandaoni zinamilikiwa na nani? Mbona hazichukuliwi hatua?

ngaiwoye

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
2,583
Reaction score
4,009
Siku hizi kutokana na mambo mengi uhitaji wa mikopo umeongezeka kwenye jamii. Hivi sasa pia kuna kampuni zinazokopesha mtandaoni kwa njia ya kijiditali, jambo ambalo ni zuri na linarahisisha mambo.

Cha kushangaza mikopo hii ni kausha damu, haifati viwango vya riba vilivyowekwa na benki kuu ya Tanzania.

Kibaya zaidi siku moja kabla ya siku ya kulipa mkopo, wanaanza kutumia meseji na kutishia na kuwatusi wateja wao. Halafu wanaanza kusambza habari za mteja na picha yake na namba kwamba wanamdai, hata kama huyo mteja ameanza kuwalipa.

Soma Pia: Kampuni za ukopeshaji zinazokiuka sheria na kanuni kwanini hazichukuliwi hatua?

Mfano mimi napigiwa naambiwa nimedhamini mkopaji na sijawahi kudhamini mtu, natishiwa, natukanwa...hivi ina maana serikali haiini hizi kampuni ikazichukulia hatua?
 
Back
Top Bottom