Karia muda wake unakwisha May, 2025. Na hatapaswa kugombea tena kwa mujibu wa katiba ya TFF. Mpaka kufikia mwakani muda wake utakapokuwa umekwisha Karia atakuwa amehudumu kwa miaka nane, ikiwq ni vipindi viwili vya miaka minne minne.
Kwa wale ambao hatukuwahi kumkubali Karia na kuchoshwa na uongozi wake, kwa sasa tuna wajibu huu.
1. Kuwa wavumilivu ili Karia amalize muda wake, tusimpe sababu ya kuvuruga mambo ili atengeneze sababu ya kuendelea kukaa pale hata mwezi mmoja mbele.
2. Tuanze kuwajadili na kutengeneza njia kwa wagombea bora wa nafasi ile sasa. Tusipofanya hivyo, machawa wa Simba, Yanga na CCM watatutengenezea wakina Karia wengine na tukajikuta tunawapa nafasi tena.
3. Tuanze kupiga kelele na kukosoa vikali ubovu wa Karia na wapambe wake ili wachokwe kabisa na kukosa sababu ya kubadilisha kanuni, katiba itakayofanya waendelee kukaa pale au kurejea kwa mlango wa nyuma kupitia uchaguzi.