Hivi kati ya Mwalimu Kashasha na Dkt Leakey nani zaidi katika uchambuzi wa soka?

Hivi kati ya Mwalimu Kashasha na Dkt Leakey nani zaidi katika uchambuzi wa soka?

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Kwa wale wapenzi wa mpira haya sio majina mageni katika uchambuzi wa soka hapa nchini.

Sasa tupige kura kwa kutoa maoni yetu kwa jinsi tunavyowafahamu hawa jamaa. Mwalimu Alex kashasha na Dr keaky Nani mkali kwenye uchambuzi wa soka hapa nchini?
 
Ndugu yangu; haya majina ni kweli ni maarufu katika uchambuzi wa soka hapa Tanzania lakini hawa ni watu wawili tofauti ambao hata katika uchambuzi huwa hawaongelei mambo yanayofanana.

Mwalimu Kashasha ni kocha na ni mtaalamu wa mpira; yeye huwa anachambua ''utaalamu'' na ''mbinu'' katika mchezo husika. Yeye hutuambia kuhusu mbinu za kimichezo, na makosa ya kimichezo yanayofanyika, na walau kuondoa utata kwa matukio yanayohitaji uchambuzi wa kitaalamu. Anafanya kazi yake vizuri sana katika upande huo na hachoshi kumsikiliza.

Dr Leakey Abdalla yeye ni mpenzi, mshabiki, mpenda soka. Uchambuzi wake hujikita zaidi katika historia na bashasha za mpira.Yeye huwa anatupa historia ya timu, historia ya wachezaji mmoja mmoja na hata matukio ya huko nyuma kuhusu timu na wachezaji; ni kawaida ya mwanandamu kupenda kusimuliwa na kuhadithiwa kwa sababu inakusogeza karibu na jambo unalosimuliwa.

Kwa walioanza kuangalia mpira zamani kidogo kwenye miaka ya 1994 - Fainali za World Cup Marekani- Dr Leakey alipata mashabiki wengi sana kwa kuwa hakukuwa na internet lakini yeye alikuwa anajua historia ya timu na wachezaji wake; watu walikuwa wanataka Dr Leakey asimulie kuliko hata kuangalia mpira wenyewe. Brazil chini ya Kapteni Dunga, Romario, Bebeto ikiibuka na ubingwa dhidi ya Italia kwa changamoto ya mikwaju ya penati; Roberto Baggio akiizamisha Italia baada ya kupaisha penati.

Na mwaka 1996 - wakati wa Fainali ya Kombe la Afrika - ilifanyika South Afrika pia Dr Leakey alifanya kazi kubwa mno ya kutusimulia na kutupa historia (mechi zilikuwa zinaonyeshwa ITV).South Africa ikiwa na wachezaji wake kama Dr Khumalo, Lucas Radebe, Tinkler na wengineo wakiifunga Tunisia kwenye fainali. Gazeti la Michezo lilikuwa Dimba na lenyewe lilikuwa linasubiri Dr Leakey aongee na wao wakaandike.

Nani bora kati yao linaweza kuwa swali lisilo na jibu kwa kuwa huwezi kulinganisha watu wanaofanya jambo moja lakini katika mtazamo tofauti.

Nikupe mfano mdogo; ripoti ya daktari juu ya kifo cha mtu aliyepigwa risasi itasomeka hivi ''sababu ya kifo ni kupoteza damu nyingi'' lakini ripoti ya polisi itasomeka ''mtuhumiwa alikufa baada ya kupigwa risasi''. Kwenye taaluma ya udaktari sababu ya kifo haiwezi kuwa ''kupigwa risasi'' kwa kuwa unaweza kupigwa risasi na ukapona, lakini ''huwezi kupoteza damu nyingi na ukapona''

Wote tunawahitaji kwa sasa maana upande mmoja tunapata uchambuzi wa kitaalamu na upande mwingine tunapata uchambuzi wa ''kihistoria'' ''kiushabiki'' na ''bashasha'' za kimpira. Wanaleta radha tofauti na tunahitaji vyote kutoka kwao.

Mpira ni sayansi lakini pia mpira ni ''interest'' na enjoyment.

Ni muda sasa kwa Watanzania hasa vijana kujifunza kumsifia mtu kwa sifa zake bila kumlinganisha na mwingine. Sio kila eneo watu wanahitaji kushindanishwa. Kuna maeneo unahitaji ''combination'' ili uweze kufurahia maisha.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom