kikoozi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2015
- 2,094
- 3,108
Ndugu yangu; haya majina ni kweli ni maarufu katika uchambuzi wa soka hapa Tanzania lakini hawa ni watu wawili tofauti ambao hata katika uchambuzi huwa hawaongelei mambo yanayofanana.
Mwalimu Kashasha ni kocha na ni mtaalamu wa mpira; yeye huwa anachambua ''utaalamu'' na ''mbinu'' katika mchezo husika. Yeye hutuambia kuhusu mbinu za kimichezo, na makosa ya kimichezo yanayofanyika, na walau kuondoa utata kwa matukio yanayohitaji uchambuzi wa kitaalamu. Anafanya kazi yake vizuri sana katika upande huo na hachoshi kumsikiliza.
Dr Leakey Abdalla yeye ni mpenzi, mshabiki, mpenda soka. Uchambuzi wake hujikita zaidi katika historia na bashasha za mpira.Yeye huwa anatupa historia ya timu, historia ya wachezaji mmoja mmoja na hata matukio ya huko nyuma kuhusu timu na wachezaji; ni kawaida ya mwanandamu kupenda kusimuliwa na kuhadithiwa kwa sababu inakusogeza karibu na jambo unalosimuliwa. Kwa walioanza kuangalia mpira zamani kidogo kwenye miaka ya 1994 - Fainali za World Cup Marekani- Dr Leakey alipata mashabiki wengi sana kwa kuwa hakukuwa na internet lakini yeye alikuwa anajua historia ya timu na wachezaji wake; watu walikuwa wanataka Dr Leakey asimulie kuliko hata kuangalia mpira wenyewe. Na mwaka 1996 - wakati wa Fainali ya Kombe la Afrika - ilifanyika South Afrika pia Dr Leakey alifanya kazi kubwa mno ya kutusimulia na kutupa historia (mechi zilikuwa zinaonyeshwa ITV). Gazeti la Michezo lilikuwa Dimba na lenyewe lilikuwa linasubiri Dr Leakey aongee na wao wakaandike.
Nani bora kati yao linaweza kuwa swali lisilo na jibu kwa kuwa huwezi kulinganisha watu wanaofanya jambo moja lakini katika mtazamo tofauti.
Nikupe mfano mdogo; ripoti ya daktari juu ya kifo cha mtu aliyepigwa risasi itasomeka hivi ''sababu ya kifo ni kupoteza damu nyingi'' lakini ripoti ya polisi itasomeka ''mtuhumiwa alikufa baada ya kupigwa risasi''. Kwenye taaluma ya udaktari sababu ya kifo haiwezi kuwa ''kupigwa risasi'' kwa kuwa unaweza kupigwa risasi na ukapona, lakini ''huwezi kupoteza damu nyingi na ukapona''
Wote tunawahitaji kwa sasa maana upande mmoja tunapata uchambuzi wa kitaalamu na upande mwingine tunapata uchambuzi wa ''kihistoria'' ''kiushabiki'' na ''bashasha'' za kimpira.
Mpira ni sayansi lakini pia mpira ni ''interest'' na enjoyment.
umeongea vizuri sana