Hivi kazi ya korodani ni nini?


Maelezo mazuri mkuu. Sahihisho dogo tu. Tezi dume haiko kwenye pumbu. Iko chini tu ya kibofu cha mkojo na kuzunguuka mrija wa mkojo, nje kabisa ya scrotal sac au pumbu. Picha hapa chini inaeleza vizuri zaidi.

In fact, ili daktari aangalie kama tezi dume imevimba au la hatomasi mapumbu bali anatia kidole kwenye rectum na kuona kama imevimba.



 
kazi ya prostate ni nini na korodani nini?
 
kazi ya prostate ni nini na korodani nini?
Korodani (gololi mbili ndani ya pumbu) ni sawa na ovaries za wanawake. Wakati ovary inatengeneza yai, korodani inatengeneza mbegu za kiume ambazo zikikutana na yai basi mtoto anatengenezwa (mimba).

Prostate gland (tezi dume) kazi yake ni kutengeneza maji yatakayolinda mbegu za kiume zinapoingia ukeni. Uke unakuwa acidic wakati wote. Prostate inatoa maji ambayo ni alkaline. Haya maji yanachanganyika na mbegu kutoka kwenye korodani kufanya manii.

Wanawake pia wana prostate gland (inaitwa SKENE'S gland) ambayo inafanya kazi sawa na prostate ya wanaume. Ukimuandaa mwanamke vizuri basi anatoa haya maji kwa wingi sana (female ejaculation au squirting - mnalowanisha mashuka). Haya maji ambayo ni alkaline pia husaidia kufanya mbegu za kiume ziishi kwa muda mrefu ndani ya uke, ambao kwa kawaida ni acidic. Wingi au uchache wa haya maji kutoka ukeni yanatofautiana kutoka mtu hadi mtu, lakini siku zote yanatoka ukeni.

I hope hii imesaidia.

********************************************************
NYONGEZA:
Nilisahau kuelezea kazi nyingine ya hizi tezi (prostate na skene's) kwa wanaume na wanawake.

Wakati wa tendo la ndoa hizi tezi zinaanza kutuna (kuvimba) kwa ajili ya maji yanayotengenezwa. Kwa kuwa mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu umezunguukwa na hizi tezi (zilizoko chini tu ya kibofu) basi zikituna hubana ule mrija hivyo kwamba huwezi tena kukojoa (mkojo wa kawaida utokao kwenye kibofu) wakati wa tendo. Nafikiri watu wanajua hali hii.
 
hapo umekata kiu kabisa
 
kaka swali la mwisho squirting yale maji huwa yanatoka wapi?katika tundu ya mkojo au ndege tunduni?
 
kaka swali la mwisho squirting yale maji huwa yanatoka wapi?katika tundu ya mkojo au ndege tunduni?
Sawa sawa na wanaume. Haya maji (female ejaculate) yanatoka kwenye Skene's gland, yanaingia kwenye mrija wa mkojo, na kutoka kwenye tundu la mkojo ukeni.
 
Sawa sawa na wanaume. Haya maji (female ejaculate) yanatoka kwenye Skene's gland, yanaingia kwenye mrija wa mkojo, na kutoka kwenye tundu la mkojo ukeni.
thanks a lot.nikiwa swali lingine takurudia mr kifyatu
 
Mkuu na ikatokea korodani moja ya kushoto inauma zaidi ya miaka mitatu na mtu ulishafanya vipimo vya ultrasound na vya mkojo bila twtizo kuonekana . Jekuna madhara?
Ahsante.
 
Mkuu na ikatokea korodani moja ya kushoto inauma zaidi ya miaka mitatu na mtu ulishafanya vipimo vya ultrasound na vya mkojo bila twtizo kuonekana . Jekuna madhara?
Ahsante.
Jaribu kuvaa chupi zenye wigo (kama boxers na sio briefs). Mimi ilinisaidia enzi hizo.

Mimi sio daktari wa binaadam. Nakushauri umuone daktari. Korodani kuuma kwa muda mrefu hivyo sio kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…