Hivi Kenya hakuna polisi , mbona wapinzani hawapigwi mabomu ?

Kenya ndo wanaikaribia dunia ya pili.ndo ujue bado Tuna safari ndefu bongoland

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha kudanganya watu wewe,Kenya unauawawa ukileta za kuleta ukitaka mifano nikuoneshe
Siku ya jumatatu vilitembea virungu vya kutosha mahakamani baada ya watu wa Odinga kulazimisha kuingia kwa wingi mahakamani,mpaka sasa mlinzi wa Odinga ana kesi ya kuchomoa bastola hadhari na kuipunga kama mwenge wa uhuru
 
Mkuu Kenya ni ya wananchi. Katiba ni ya wananchi na walioko madarakani wapo kwa niaba ya wananchi.

Kwetu siyo hivyo.

Kwetu nchi ni watawawala. Katiba hawana haja nayo. Kuna mhimili uliochimbiwa zaidi. Polisi wa kulinda watawala. Mahakama zinawajibika kwa watawala.

Kimsingi kwetu ni rojo rojo kwa maneno ya mkulu mwenyewe hakuna kuleta fyoko fyoko.
 
Kipindi kile cha power sharing nadhani some Institutions ziliundwa vyema na Katiba yao mpya imestreamline mambo mengi. Tatizo huku kwetu mtu mmoja amepewa power ya kuwafanyia maamuzi watu wote. Nyerere (RIP) aliliona hili kitambo ila akaamua kuliacha lilivyo.
 
Ushauri - Kenya ijiondoe EAC , haifanani na wanachama wengine , ikibaki itajichafua .
baada ya matokeo kutangazwa palizuka maandamano kisumu na nairobi,polisi walitumia nguvu,watu walipoteza maisha,hukufuatilia habari au kipindi hiki ulikua unamnyoa maalim ndevu!!?
 
God plz put some sense into mkulus mind that once we hit the streets africa na dunia haita amini kitakacho tokea haki haiombwi ......
 
Mafunzo ya police wa Kenya ni tofauti na mafunzo ya polisi wa Tanzania.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
aliliona au aliliasisi yeye na halikuwahi kumkera,hata hivyo demokrasia kwenye nchi ambayo mbumbumbu ni wengi kuliko werevu..ni sumu tamu
 
Wakenya walipigana kwanza,wakapelekana ICC na matunda yake ndiyo haya yanayotokea leo.

Tanzania tunasubiri HURUMA ya SERIKALI na CCM...
 
Baada ya kulazimisha......... Hapa kwetu mtu kavaa tsheti ya ukuta anajiendea shambani anaitwa mchochezi, sasa sijui anaenda kuchochea mazao yasiote?
 
Simple,wapinzani wa Kenya si wachumia tumbo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…