Hivi Kigoma kukoje? Wakulima wanakaa foleni wiki nzima kusubiri mbolea ya Ruzuku

Hivi Kigoma kukoje? Wakulima wanakaa foleni wiki nzima kusubiri mbolea ya Ruzuku

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kigoma wanaishije lakini?

Nimeshuhudia kupitia ITV habari Wakulima wanalalamikia mbolea ya Ruzuku wanaifuata mjini na wakifika wanakaa foleni zaidi ya Siku tatu ndio unauziwa

Ndio najiuliza Kigoma ni Tanzania kweli?
 
Mkuu usishangae maana inawezekana hiyo hali utaanza kuiona pia katika mikoa mingine tofauti na Kigoma

Saizi kuna mabadiriko ya mfumo wa kuuza Mbolea, mwanzo ilikuwa ni ruhusa Kwa Duka lolote la pembejeo kuuza Mbolea kikubwa awe na vibali tu

ila kwa sasa hali ni tofauti, kwani kuna mawakala wa uuzaji wa mbolea hivo kufanya katika maeneo mengi mbolea kuwa hakuna kabisa au kupatikana kwa shida

Mfumo wa sasa unataka anaeuza Mbolea awe ni wakala na anaenunua/mkulima awe amesajiliwa ili kuweza kununua mbolea kutoka kwa wakala

Kuna baadhi ya maeneo Dar na Pwani saizi hakuna kabisa mbolea na hali hiyo imepelekea biashara ya uuzaji wa pembejeo kuwa ngumu kupita maelezo
 
Hiyo hali kila mahali siyo kigoma tu, umesahau kuna mtu alifariki kwa uchovu wa kusubir mbolea za ruzuku kwenye foleni. Serikali haijaweka mpango mzuri wa upatikanaji wa mbolea.
 
Back
Top Bottom