Mkuu usishangae maana inawezekana hiyo hali utaanza kuiona pia katika mikoa mingine tofauti na Kigoma
Saizi kuna mabadiriko ya mfumo wa kuuza Mbolea, mwanzo ilikuwa ni ruhusa Kwa Duka lolote la pembejeo kuuza Mbolea kikubwa awe na vibali tu
ila kwa sasa hali ni tofauti, kwani kuna mawakala wa uuzaji wa mbolea hivo kufanya katika maeneo mengi mbolea kuwa hakuna kabisa au kupatikana kwa shida
Mfumo wa sasa unataka anaeuza Mbolea awe ni wakala na anaenunua/mkulima awe amesajiliwa ili kuweza kununua mbolea kutoka kwa wakala
Kuna baadhi ya maeneo Dar na Pwani saizi hakuna kabisa mbolea na hali hiyo imepelekea biashara ya uuzaji wa pembejeo kuwa ngumu kupita maelezo