Mkulu Balantanda, asante kwa ufafanuzi wako. Nikweli mapokeo tuliyonayo sii mazuri sana juu ya kilimo. Mtumwingine akiulizwa unafanya kazi gani atakwambia sinakazi. Kimsingi wawezakutamtu huyu labda anajishughurisha na kilimo cha bustani mfano lakini kwake kuwa na kazi ni kufanya kazi kwenye maofisi tuliyo yazoea bilakujua kuwa hata bustani ni office pia.
Kwa upande wa mkulu Exaud J. Makyao swali la je kilimo ni kazi au la na kwanini watu hawajishughulishi kuomba kazi za kilimo. Nadhani kwa lugha nyepesi mkuu utakuwa shahidi, shule nyingi hasa za kijijini mwanafunzi akifanya kosa basi adhabu kuu atakayopewa utakuta ni kulima, kufyeka nyasi, kupalilia mazao fulani, na shule niliyosoma mimi ilikuwa kung'oa visiki na kupasua kuni. Kaka adhabu kama hizi zinamfanya mtu aone kilimo ni adhabu na akichukie kabisaa.
Mwenye uzoefu mwingine atuhabalishe