Hivi kipa wa Simba analaumiwa kwa lipi?

Hivi kipa wa Simba analaumiwa kwa lipi?

Goli la leo kosa kalifanya Chama kwa kushindwa kukimbia na kukaa mbele ya mshambuliaji kumkinga asipige mpira. Goli la Zambia alilisabababisha Muzamiru kwa kutofanya jukumu lile lile.
N.B:Goli la leo linafanana na goli la kwanza Mayele alilofunga ngao ya jamii. Makosa kama haya kwa wenzetu hasa Bundesliga ukiyafanya lazima ufungwe
Mkuu kwa mtu aliye anza kushabikia mpira ukumbwani hawezi kulijua hili ,alafu kati ya makipa ambao huwa wanafungwa magoli ya kifala hapa tz manula anaongoza.
 
Tena Golikipa mwenyewe MSH3ENZI wamempa Miaka Miwili.

AONDOKE

magolikipa walitakiwa kuja Simba wote wameshindikana kwa sababu ya Simba kuchagua Rangi.

1. Walimuacha BONGE la Goal keeper WA Cameroon.

2. Walimuacha Golikipa mzuri akaenda KITAYOSE.
 
Ukweli ndo huooo...
Acheni kujadili mpila...
 
Kosa sio la kipa. Kulikua na shimo mbele ya mabeki kiasi jamaa alitaka kutoa pass alivyoona hafuatwi akasogea tena na tena mpaka alivyoona kaupenyo akapitisha mpira. Kipa alikuja kushtuka kashachelewa.

Kipa analaumkwa labda kwa sababu; kwa nn ashindwe kuokoa mpira kuficha mapungufu ya viungo na beki?

Huu msimu nauona simba upepo uko upande wake. Mnajua simba ni timu mbovu kweli lkn cha ajabu inapata matokeo na ngao ya jamii wanayo. Waliipateje, inabaki kua miujiza.

Hivi nyie yanga, kama mlishindwa kumgonga simba goli 5 finali ngao ya jamii, lini mtakuja kumfunga?
 
Kwakweli saa nyingine huna nashindwa kujua iwapo mashabiki wa mpila wa Tz Wana uwelewa gani wa mpila zaidi ya kufuata mikumbo na ushabiki.

Sasa hivi naona kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wa Simba wanamshambulia na kumlaumu kipa eti kafungwa goli la kizembe , hivi kwa mtu anaye jua mpila kabisa kipa anahusikaje kwenye hilo goli?

Yaani mchezaji anapokea mpila kutokea karibia mita 35 kutoka kwenye goli ana ukokota mpila viungo wana muangalia tu, anaukokota mpaka nje kidogo ya box mabeki wamemuangalia tu, bado ana endelea kuukokota mpaka katikati ya mabeki wa 4 wa simba anapiga shuti wamemuangalia, alafu anatokea mtu ana mlaumu kipa , na mkumbuke hata lile goli la pili alilo fungwa simba akiwa zambia na lenyewe mshambuliaji alilipiga akiwa katikati ya mabeki kama watatu.

Kwanza kipa alikuwa amekingwa na mabeki na hilo shuti lilikuwa na kushutukiza na lilikuwa na kasi hata angekuwa nani pale ange fungwa tu wana simba tuache visingizio na kutaka kumtwisha kipa wakati timu nzima kiujumla ina kiwango cha hovyo.

Wanao takiwa kulaumiwa ni viungo na mabeki walio shindwa kutimiza majukumu yao, hivi timu iliyo jaa viungo inawezaje kumruhusu mchezaji akokote mpila akiwa huru kabisa kwa muda mrefu namna hiyo aisee au simba imetogwa?

Tatizo hapo simba ni kocha kiufupi mpila ni mchezo wa wazi kwa mpila unachezwa na simba unadhihirisha na unaonesha kabisa ya kuwa kocha timu imemshinda ,viongozi wa simba waache kijificha kwenye kichaka cha timu kupata matokeo simba inacheza mpila wa hovyo kabisa.
Mpila
Mpila
Mpila

Lugha gani hii?
 
Washabiki wengi wanakariri, uzembe wa kukaba na mpira kudunda mbele ya kipa. Timu nzima ilicheza ovyo kuanzia kocha.
 
Kosa sio la kipa. Kulikua na shimo mbele ya mabeki kiasi jamaa alitaka kutoa pass alivyoona hafuatwi akasogea tena na tena mpaka alivyoona kaupenyo akapitisha mpira. Kipa alikuja kushtuka kashachelewa.

Kipa analaumkwa labda kwa sababu; kwa nn ashindwe kuokoa mpira kuficha mapungufu ya viungo na beki?

Huu msimu nauona simba upepo uko upande wake. Mnajua simba ni timu mbovu kweli lkn cha ajabu inapata matokeo na ngao ya jamii wanayo. Waliipateje, inabaki kua miujiza.

Hivi nyie yanga, kama mlishindwa kumgonga simba goli 5 finali ngao ya jamii, lini mtakuja kumfunga?
Mkuu lakini anaye takiwa kumlinda mwenzake ni mabeki na sio kipa kulinda mabeki.
 
Back
Top Bottom