Hivi Kipchoge anaweza pia mbio za 100 m?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Huyu mkimbiaji maarufu duniani R. Kipchoge, anaweza pia mbio za 100m au yeye ni hizo za muda mrefu tu? Ana rekodi yoyote ya 100 m?
 
Mtu anayekimbia mbio kilomita 42 chini ya masaa mawili ashndwe mita mia???? Hehehe
Au labda unauliza kama anaweza kuwashinda akina Bolt wale wakimbiaji wa mita mia, hapo sitegemei awashinde maana kila aina ya mbio hutegemea maandalizi tofauti.
 
Ndicho nilichomaanisha, kukimbia 100 m kila mtu anaweza.
 
Atamaliza ila top 10 sidhani
 
Mtu anayekimbia mbio kilomita 42 chini ya masaa mawili ashndwe mita mia???? Hehehe
Au labda unauliza kama anaweza kuwashinda akina Bolt wale wakimbiaji wa mita mia, hapo sitegemei awashinde maana kila aina ya mbio hutegemea maandalizi tofauti.

Haiko hivyo. Ukiwa unakimbia mbio ndefu wewe ni wa ndefu tu. Ukiwa unakimbia mbio fupi ni fupi tu. Mbio za kina Hussain Bolt zinahitaji nguvu, kasi, misuli mikakamavu.
 
Mbio za mita mia ni sprinting. Zinahitaji strengthh na muscles ili uweze kutumia your maximum strenght with in a very short period of time kumaliza mbio hizo fupi kabisa.. kama kina bolt..Lazma uwe na misuli na maguvu na uzito pia wa misuli (muscle weight) ndio maana utakuta bolt ana kilo karibu 90 wakati kipchoge ana kilo 57.... mbio ndefu za kina kipchoge zinahitaji endurance... uwezo wa kuhimili kukimbia at a constant pace kwa muda mrefu, hii haihitaji misuli wala weight maana utachoka mapema.. inahitaji mwili mdogo na energy ya kutosha kuweza kumaintain pace yako...mazoezi pia wanayofanya ni tofauti.. sprinters wako kutengeneza strength zaidi while marathoners wao wanatrain for emdurance zaidi... lishe zao pia ni tofauti...
Kipchoge anaweza kusprint, but hatoweza kushinda.. na pia bolt anaweza kucheza marathon na yeye pia hatashinda
 
Haiko hivyo. Ukiwa unakimbia mbio ndefu wewe ni wa ndefu tu. Ukiwa unakimbia mbio fupi ni fupi tu. Mbio za kina Hussain Bolt zinahitaji nguvu, kasi, misuli mikakamavu.

Sasa mbona unahemka kwani nimesema chochote tofauti, kila aina ya mbio huhitaji maandalizi tofauti, akiamua kufanya mita 100 itabidi atelekeze za 42km maana maandalizi ya kimwili ni tofauti kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…