Hivi kipofu huwa anaota nini??

Anaota ndoto ambazo mazingira yake yana mwanga au yakiwa na giza?
 
Niseme tu kwamba inategemea na kipofu ana uelewa gani.
Nina girfriend,ni kipofu. Lakini ana akili usipime.
Nilichojifunza kwakwe,kwanza nilimuuliza anawezaje kutofautisha usiku na mchana. Alichonijibu ni kwamba kupitia upepo kuvuma, sauti za ndege, magari na vitu vingine.
Pia nimekuja kugundua hawa watu wana sensi ya 6_ya pekee
Ukiwasha taa anajua, ukizima anajua pia. **** kuna mwanga au giza,anajua.
Huyu naemuongelea, anakaa peke yake,naanajipikia,anajifanyia usafi. Kasoma pia.
Sasa kwenye swala la ndoto,
Anapoongea na watu,anaposikiliza radio, haya yote hukaa kwenye ubongo na kujirudia. Maana ukiangalia mantiki ya ndoto,ni marudio ya vitu ulivyoviona, ulivyosikia au ulivyofikilia.

Huyu ni mtumiaji mzuri wa simu na kompyuta. Hataona picha, lakini meseji atasoma na ataandika.
Hawa viumbe ni wa ajabu asikwambie mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…