Hili swali najua wengi wetu tunajiuliza sana, lkn ukilitafakar kisayansi zaid utaelewa kuwa hta vipofu nao huota....
Kwanza ndoto nyingi ni Imagination yan mambo ya kufikirika na source kubwa ni kutoka kwenye ubongo, kwahyo ss kama kipofu lazima atakua na njia ya utambuzi wa vitu either kwa kugusa, kusikia, kunusa au hata kulamba mana hizo ni njia kuu za ufahamu ukiondoa ya macho ambayo hawana,
Ss akiingia kulala ubongo hufanya kazi kubwa ya kurudia matukio ya mchana na kuumba vingine vingi hapo ss ndo ndoto nzima hutimia,
Natumain nimeeleweka kidogo....nikipata mda ntaweka uzi juu ya hili swala.
Lakin ngoja niwaache na challenge kidogo...
Je unauhakika gani jinsi uionavyo rangi ya blue ndivyo na mimi au mwingine aionavyo hivyo hiyo rangi ya blue!?
Tafakari pia tupeane majibu hapa....
Niseme tu kwamba inategemea na kipofu ana uelewa gani.
Nina girfriend,ni kipofu. Lakini ana akili usipime.
Nilichojifunza kwakwe,kwanza nilimuuliza anawezaje kutofautisha usiku na mchana. Alichonijibu ni kwamba kupitia upepo kuvuma, sauti za ndege, magari na vitu vingine.
Pia nimekuja kugundua hawa watu wana sensi ya 6_ya pekee
Ukiwasha taa anajua, ukizima anajua pia. **** kuna mwanga au giza,anajua.
Huyu naemuongelea, anakaa peke yake,naanajipikia,anajifanyia usafi. Kasoma pia.
Sasa kwenye swala la ndoto,
Anapoongea na watu,anaposikiliza radio, haya yote hukaa kwenye ubongo na kujirudia. Maana ukiangalia mantiki ya ndoto,ni marudio ya vitu ulivyoviona, ulivyosikia au ulivyofikilia.
Huyu ni mtumiaji mzuri wa simu na kompyuta. Hataona picha, lakini meseji atasoma na ataandika.
Hawa viumbe ni wa ajabu asikwambie mtu.