Hivi kugegeda nini na hili neno limenzaia wapi?

Hivi kugegeda nini na hili neno limenzaia wapi?

hapo tunatumia tafsida tumepunguza ukali wa maneno,ila maana halisi ya kugegeda ni kutafuna kitu kitamu kwa raha zote

Hata mimi ndivyo ninavyojua, mzizi ni Mrima, hususan Kiswahili cha kutoka Kizaramo.

Kugegeda ni kutafuna, mathalani kutafuna muhogo kwa mapande makubwa na kwa kufanya sauti kubwa .
 
lugha huzaliwa hukua na hatimaye hufa, neno kugegeda sasa hivi linatumika kivingine kabisa n vijana wa kileo wakimaanisha kufanya ngono
 
Hata mimi ndivyo ninavyojua, mzizi ni Mrima, hususan Kiswahili cha kutoka Kizaramo.

Kugegeda ni kutafuna, mathalani kutafuna muhogo kwa mapande makubwa na kwa kufanya sauti kubwa .
Hata sisi kule mjasani na Pongwe Tanga tunatumia neno hilo wakati tunatafuna mhogo wa kibanda meno au mahiza.
Ukigegeda kitu ni kama vile unang'ofoa lakini ukiwa na hisia njema na halali.

Kwingineko siku hizi linatumika, ah ! anyway
 
Back
Top Bottom