Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nchi ya Ukraine imeingia kwenye vita kwa nia ya kujiunga na kuongoza ushirikiano na umoja wa NATO jambo ambalo Urusi hawalitaki. Katikati ya vita hivi na madhara makubwa kwa nchi ya Ukraine yakishuhudiwa kote duniani,bado kuna mataifa jirani na Urusi kama vile Sweden na Finland zimekuwa zikijadili na kuongeza harakati za kujiunga na umoja huo unaoichukiza nchi ya Urusi.
Ni zipi faida za kujiunga na umoja huo kiasi cha mataifa ya Ulaya Mashariki, jirani na Urusi kujiweka hatarini kuharibu nchi zao.Kwa upande mwengine twaweza kujiuliza kwanini nchi nyingi zina kiherehere cha kujiunga na NATO ilhali watu wanaoishi Urusi wanaonekana kuishi maisha bora zaidi kuliko wanaoishi mataifa ya NATO.