Hivi kumiliki 10m mtu unaweza kujiita milionea kweli?

Mkuu kumbe anajiita, imefikia hatua tunaanza kuchaguliana na majina ya kujiita! Maisha yenyewe mafupi haya, acha ajipe raha na amani ya moyo mwenyewe.

Tujibu swali lako je mwenye milioni 10 pesa taslimu za kitanzania anafaa kuitwa milionea!
Milionea ni mtu yoyote anaemiliki aidha pesa taslimu ama mali zenye thamani ya kufika milioni
Sasa huyuo mwamba kwa pesa zetu za madafu acha ajimwambafai tu.

Ila kwa duniani hawezi kuitwa milionea sababu pesa hiyo ikithaminishwa kwenye pesa yenye nguvu ulimwenguni hiyo tsh m10 yake inakuwa kama dola elf 4 na upuuzi hivi!!

Kwa pesa zetu za madafukina bakheresa,manji, marehemu mengi na wengineo ni mabilionea ila kwa pesa za duniani huko ni mamilionea tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akijiita hamna tatizo[emoji23][emoji23][emoji23].

Ila ili uwe millionaire inatakiwa mali zako ziwe na thamani ya kwanzia 1M (dollars or Pounds).
Hiyo ni interpretation yako mkuu.. ikiwa kama wewe currency yako siyo dola kwani hauruhusiwi kujiita milionea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…