Hivi kumiliki gari ya safari ndefu Kama Toyota Prado kwa safari fupi za mjini ni akili au ujinga?

Usipoombwa ni kimbelembele.
Unayemshauri akikuuliza "kwani nilikuomba ushauri?" unazodoka.
Si kila unayefikiri hajui unayotaka kumshauri hajui, wengine wanajua, ila hawajali.
Kimbelembele ni kumpangia matumizi hela yake si kumshauri matumizi bora ya hela yake!.
Elimu haiihitaji kuombwa, inahitaji tolewa ataikataa kwa wakati huo lakini hataikataa daima.
Si kila anayejua anajua kweli halisi!.
 
Hizi gari ndogo zilitengenezwana wenzetu kwa ajili ya mizunguko mjini na kupinguza uchafuzi wa hewa moshi mjini.

Wajapani sio masikini kwamba walitengenezewa ist au vitz kwa kubana matumizi ya mafuta. Wenzetu wanathamini sana mazingira na hewa safi.
 
Aiseee.....mtoa mada naona umepewa za uso kinoma..
Anyway, mtazamo wangu mimi ukitaka kumiliki gari, miliki gari linaloendana na kipato chako,

Lakini pia itapendeza gari unalomiliki limudu safari zote, mjini na upcountry..

So mwenye uwezo wa V8 mjini ewalaa...mwenye uwezo wa ist,vitz ewalaa...

Kuna unapofikia...

Usilazimishe kuinama ili ukune usipopafikia....Utatujambia..
 
Nakazia
 
Usipoombwa ni kimbelembele.

Unayemshauri akikuuliza "kwani nilikuomba ushauri?" unazodoka.

Si kila unayefikiri hajui unayotaka kumshauri hajui, wengine wanajua, ila hawajali.
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Toyota Prado ni gari mahususi ambayo imetengenezwa kwa ajili ya safari ndefu Sio mizinguko mifupi fupi ya mjini.Hivi mtu kumiliki Hilo dude kwa safari za mizunguko ya mjini Ni akili au ujinga? Sio matumizi mabaya ya pesa ?
Mbona Lumumba hapo mnamiviet kibao.acha unafiki we kibwengu
 
Kumpangia mtu atumie gari gani ni akili za kipumbavuh. Pesa yangu, gari langu, sikuombi chochote unanipangia nitumie gari gani mjini? Ulaya na marekani wanatumia hadi train kwenye mizunguko ya mjini badala ya daladala...kwa akili yako wewe si ungesema train ni za kwenda mikoani?

Prado imeandikwa wapi kuwa ni gari maalum kwa safari?yaani gari ya mizunguko ya kawaida tu wewe unasema ya safari? Ukiwa maskini unaweza mpaka pangia wenzako bajeti...ukosefu wa fikra. Mtu hata akiamua atumie helcopter kwendea kazin ni uamuzi wake. Achen kuwaza kimaskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…