Hivi kuna chama ambacho kinaweza kuitoa CCM madarakani?

Hivi kuna chama ambacho kinaweza kuitoa CCM madarakani?

Huwa najiuliza ni chama ganii chenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, kwa sababu CCM ni kama Mandonga Ukimshinda ni kama amekushinda, na akishinda ameshinda.

Namuomba Mungu anijalie afya njema ili siku moja niweze kushuhudia kwa macho yangu CCM ikipigwa knockout na chama chochote cha upinzani.
Wakina Dr. Slaa, Tundu Lissu, Mwabukusi, Mdude, Mpina wakienda kuteka moja ya vyama dhaifu kama UDP au hata CHAUMMA wanaweza kuchukua hii Nchi kwasasa CCM siyo tena chama cha siasa hakina wanachama wakutosha kimejaa watu maslahi.
 
CHADEMA iko well organised ndio chama cha upinzani tishio kwa CCM. Uchaguzi huru na wa haki ukifanyika, asubuhi mapema CHADEMA inashinda ushindi mnono na kuipeleka CCM mapumzikoni nacho kiwe chama cha upinzani
 
hata watoa taarifa wote wakiungana hawatafua dafu.
Yaani miongoni mwa mambo ambayo hayawezekani duniani basi ni pamoja na hiki....
Ungekuwa unajua Mungu yupo usingesema haya,Mungu akiamua kila kitu kinawezekana.
 
Kuna race ndani ya ccm wakishakufa wote chama kitaaondoka bila chenga

Kikwete race
Makamba race
Kinana race
Rostam race
Mwinyi race
Nape race
Hawa wote wanakilinda chama ili kiwalinde uchafu wao waliotuibia umma hivyo hutumia nguvu kubwa mno........soon
 
Hakuna chama kitakachokuja kuitoa CCM madarakani kwa njia ya kura katu katu labda kwa njia nyingine.
Viongozi wa selikari na chama wanaishi maisha ya daraja la peponi duniani(hasa wa ngazi za juu). Wale matop wote kwenye vyombo vya usalama/Dora, spika wa bunge na wasaidizi wake, mawaziri ,wakuu wa mikoa na wilaya,Wakurugenzi na watu wao wote ambao wameshikilia idara muhimu nk. Jaribu kufuatilia maisha Yao ndio utaelewa kitu nachokisema hapa.

kwa maisha ya anasa wanayoishi kazi Yao kubwa ni kuhakikisha wanayoishi maisha hayo milele daima kizazi chao choteeeeeeee!! So kusema eti chama kije kiwatoe kwa njia ya kura ni uongooooo! Watatumia Kila njia kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani na kuitafuna nchi ipasavyo.

kwa mfano maisha anayoishi spika wa bunge, lile kasiri lake lenye Kila aina ya udambwi udambwi eti Leo from no where na vikaratasi vya kura umwambie waachie Dora.

Watanzania sisi wenyewe ni waoga balaa hata tukiona hapa tumeibiwa wazi wazi hakuna wa kwenda kuhoji wizi huo Wala kusema fyoko, kibaya zaidi watawala Hawa washaujua udhaifu huu wa Watanzania.Wanajua hata tukifanya hivi ama vile hakuna wa kuja kutuhoji Wala kuandamana, kuandamana Yao ni Jf basi mambo yanaisha😂
Sasa kwa style hiyo unaitoaje CCM madarakani??
 
Kuna race ndani ya ccm wakishakufa wote chama kitaaondoka bila chenga

Kikwete race
Makamba race
Kinana race
Rostam race
Mwinyi race
Nape race
Hawa wote wanakilinda chama ili kiwalinde uchafu wao waliotuibia umma hivyo hutumia nguvu kubwa mno........soon
Mkuu unawaza kwa kutumia Nini? Unadhani hiyo race itakufa lini? We huoni kbs hao watu wanalisishana kizazi kwenda kizazi?
 
Back
Top Bottom