Hakuna chama kitakachokuja kuitoa CCM madarakani kwa njia ya kura katu katu labda kwa njia nyingine.
Viongozi wa selikari na chama wanaishi maisha ya daraja la peponi duniani(hasa wa ngazi za juu). Wale matop wote kwenye vyombo vya usalama/Dora, spika wa bunge na wasaidizi wake, mawaziri ,wakuu wa mikoa na wilaya,Wakurugenzi na watu wao wote ambao wameshikilia idara muhimu nk. Jaribu kufuatilia maisha Yao ndio utaelewa kitu nachokisema hapa.
kwa maisha ya anasa wanayoishi kazi Yao kubwa ni kuhakikisha wanayoishi maisha hayo milele daima kizazi chao choteeeeeeee!! So kusema eti chama kije kiwatoe kwa njia ya kura ni uongooooo! Watatumia Kila njia kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani na kuitafuna nchi ipasavyo.
kwa mfano maisha anayoishi spika wa bunge, lile kasiri lake lenye Kila aina ya udambwi udambwi eti Leo from no where na vikaratasi vya kura umwambie waachie Dora.
Watanzania sisi wenyewe ni waoga balaa hata tukiona hapa tumeibiwa wazi wazi hakuna wa kwenda kuhoji wizi huo Wala kusema fyoko, kibaya zaidi watawala Hawa washaujua udhaifu huu wa Watanzania.Wanajua hata tukifanya hivi ama vile hakuna wa kuja kutuhoji Wala kuandamana, kuandamana Yao ni Jf basi mambo yanaisha😂
Sasa kwa style hiyo unaitoaje CCM madarakani??