Hivi kuna Frederic Mwakalebela wangapi nchi hii?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Habari za mda huu wadau wa JFsport,

Naomba anaefahamu hili suala atudadavulie kidogo kuna mwakalebela wangapi hapa Tz? Je, huyu makamu mwenyekiti hovyo wa yanga ndio yule aliekuwa kijana smart pale TFF ya mzee Tenga? Kama ndio yeye kalishwa nini, mbona kawa mpuuzi hivi?

Hivi kweli yule mwakalebela wa TFF ya Tenga angeweza kufanya yafuatayo?

1/Kukataa nembo ya mdhamini kisa rangi nyekundu
2/Kumpa millage kubwa kit supplier kuliko main sponsors
3/Kumfukuza Zahera bila sababu
4/Kuongoza kundi la usajili ovyo ovyo bila maelekezo?
5/Kujihusisha na tetesi za usajili kabla ya dirisha (kesi ya Chama)
 
Mwakalebela means badilika badilika..Huyu zamani alikuwa David mwakalebela na alikua na busara sana akicheza beki ya kulia baadae akabadilika akawa frederick mwakalebela akawa pale TFF baadae ubongo ukatikisika..akaenda yanga akiwa kama Dunia mwakalebela na baadae atabadilika ataenda lipuli kama mtozeni mwakalebela .. tuvute subira bado tutashuhudia miujiza sana toka kwa huyu kiumbe mweusi kama mkaa
 
Huyo devid mwakalebela alicheza timu ganii?
 
kuna wakati baadhi ya watu huonekana smart kwa kuwa wanakuwa nyuma watu smart lakini wanapokuwa peke yao na wanatakiwa kufanya wao maamuzi ndo unaona mapungufu yao lakini pia tuone labda kateleza kwa hili ya chama
 
tz1
 
Kiukweli hata mimi binafsi napata shida sana na huyu Mwakalebela wa Yanga. Baada ya kupata taarifa kuwa Mwakalebela ni mojawapo wa viongozi wa juu kabisa wa Yanga nilifurahi sana nikijua sasa ataleta changamoto mpya katika soka la Tanzania kutokana na historia yake ya kufanya kazi TFF na mtu mweledi sana Leodgar Tenga.

Nilianza kupoteza imani naye kama kiongozi mweledi pale alipoaanza kushabikia vitu vidogo kama nembo ya mdhamini na kipensi cha Zahera wakati ambapo Yanga ilikuwa inapita kipindi kigumu cha ukosefu wa fedha za kuendesha timu. Yeye kama kiongozi nilitegemea apambane na mambo makubwa ya namna ya kupata fedha za uendeshaji wa timu kwa wakati ule ambapo Yanga ilikuwa haina mdhamini.

Kwa vyovyote iwavyo Mwakalebela huyu wa sasa ndio "original" yule wa TFF ni feki na inaonekana bosi wake Leonard Tenga alikuwa anamfichia madhaifu yake mengi ya kiuongozi ambayo tunayaona leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…