Hivi kuna kipengele cha ku-attach affidavit unapofanya maombi Bodi ya Mikopo (HESLB)?

Hivi kuna kipengele cha ku-attach affidavit unapofanya maombi Bodi ya Mikopo (HESLB)?

Meditator

Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
73
Reaction score
117
Habari wanajamvi,

Kama kichwa cha habari kinavo jieleza tajwa hapo awali.

Mimi ni kaka na nina wadogo zangu wawili, mmoja kamaliza Kidato cha sita mwaka huu na mwingine yupo Kidato cha nne. Mi Sina elimu kubwa sana kitu ambacho huwa na wapambania sana madogo wasome wafike mbali ili watimize ndoto zao ingawa na jua suala la upatikanaji wa ajira huwa ni msalaa siku zote pia ni jambo la Bahati.

Tuingie kwenye mada husika iliyo nileta hapa. Nipo kwenye mchakato wa kumuombea dogo mkopo wa chuo sasa nilikuwa nauliza kwa yeyote anayefahamu kama kuna kipengele ambacho unaweza ku-attach Affidavit wakati wa Maombi ya mkopo HELSB.

Muwe na mchana mwema.
 
Zifuatazo ni nyaraka muhimu za kuambatisha kwenye maombi ya mkopo: –

  1. Cheti cha kuzaliwa kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji kutoka Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji kutoka Tanzania Bara;
  2. Vyeti vya vifo vya wazazi kuthibitisha uyatima kutoka mamlaka husika, ZCSRA kwa waombaji waliozaliwa Zanzibar au Namba ya Uhakiki (verification number) kutoka RITA kwa waombaji waliozaliwa Tanzania Bara;
  3. Barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kuzaliwa kwa waombaji waliozaliwa nje ya nchi. Kwa mwombaji ambaye mzazi wake amefariki nje ya nchi anapaswa kuwasilisha barua kutoka RITA au ZCSRA kuthibitisha taarifa za kifo.
  4. Fomu ya Kuthibitisha Ulemavu wa mwombaji au mzazi wake iliyoidhinishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) au Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO);
  5. Namba ya kaya ya Mnufaika kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuthibitisha ufadhili wa kiuchumi alioupata mwombaji wakati wa elimu yake ya sekondari.
 
Hiyo haitajiki, kinachohitajika ni application code baada ya kuhakiki cheti cha kuzaliwa kule RITA
 
Back
Top Bottom