Hivi kuna kuwa na 'database' ya watu wanaostahili kuteuliwa na Rais?

Hivi kuna kuwa na 'database' ya watu wanaostahili kuteuliwa na Rais?

Ukiangalia teuzi za rais ni kama kuna list ya watu ambayo huwa tayari imeandaliwa kwaajili ya kuteuliwa. Yaani teuzi zinawazungukia wale wale.

Unakuta mtu akikosa ubunge au uwaziri atapata uRC, DC, DAS, DED au ukatibu mkuu. Mwingine unakuta alishapita vyeo vingi sasa kesha anza maisha mapya Mara unasikia anapewa uDAS ghafla tena anabadilishwa kuwa RC.

Mwingine unakuta alikuwa na vikashfa awamu zilizopita ghafla unashangaa ni RC tena. Wengine unakuta ni watoto wa viongozi wastaafu au waliokufa.

Yaani kuna watu wanaishi kwa kubadilishiwa vyeo. Mwingine unakuta ni mteule wa kudumu toka enzi za baba wa taifa. Teuzi nyingine kama hizi za maRC unakuta ni kuhamishana tu wale wale.

Sasa unajiuliza hivi wenye sifa hakuna kabisa hadi kuanza kurudia rudia hata wastaafu? Ndipo nikawaza kwamba inawezekana kuna data base ya wateule ambao huwa wanasubiri muda tu wa kukamata vyeo vyao.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Au nasema uwongo ndugu zangu?

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
Ndio maana hata wanaua watu wakati wa chaguzi i watu wao wapate madaraka. Hawafanyi vule kujifurahi. Wanajua future zao.
 
Hili ndilo Jibu sahihi kabisa,labda niongezee.
1.Wakuu wa Mikoa/na Wilaya-vetting zinafanywa na watu wa usalama wa chama na kanzi data ni huko huko CCM.
2.Wakurugenzi-Kanzi data na vetting ni TAMISEMI.
3.Makatibu wa Kuu wa Wizara/Katibu Tawala Mikoa na Wilaya/Wakurugenzi wa Taasisi za Serikali na mashirika ya umma-kanzi data ni Ofisi ya Rais-UTUMISHI
tiss-ccm. Nje ya hapo endelea kulima mahindi Dumila.
 
Back
Top Bottom