Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kuna kitu ambacho siyo cha kawaida, ambacho sijawahi kukiona katika miaka ya nyuma katika tawala zilizopita, kwa kuyabakiza mabango kwa maelfu yanaendelea kuwepo sehemu mbalimbali nchini, wakati uchaguzi ushakwisha!
Mabango hayo yalitengenezwa maalum kwa ajili ya uchaguzi mkuu pekee na kwa kuwa uchaguzi huo umekwisha, mabango hayo hayastahili kuendelea kuwepo nchi nzima.
Kwanza tujiulize mabango hayo yanatuhumiza wananchi tumchague Magufuli ili aendelee na kipindi kingine cha miaka 5.
Magufuli, ambapo tayari
Tume ya uchaguzi imemtangaza Rais Magufuli kuwa kashinda kwa kishindo, je kuna sababu gani ya kuendelea kuyatundika mabango hayo?
Ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi na kumfanyia "promo" Rais Magufuli, kwa kuwa hayo mabango yalikuwa ni kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliopita pekee na kwa vile uchaguzi huo umeshapita, sioni sababu ya kuendelea kuyatundika mabango hayo sehemu mbalimbali nchini.
Kwanza uchaguzi wenyewe umekuwa ukilalamikiwa mno na vyama vya upinzani nchini na Jumuia ya kimataifa kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na haki na ulijaa udanganyifu wa hali ya juu, kiasi ambacho hauwezi kuwa na "credibility" ya kuuita kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.