Hivi kuna madhara gani kuacha pombe ghafla?

Fanya mazoezi kula matunda sana na epuka kuwaza na kutembelea vijiwe vya pombe. Chagua kitu kingine mbadala
Ninafanya mazoezi nakula matunda na pombe nakunywa weka picha ya mwili wako hapa na mimi niweke kama mlevi🤣🤣 tuone mwenye afya njema
 
Kuna jamaa wakati anaacha pombe alikua usiku anakurupuka analia huku ananyoosha kidole dirishani anatuambia angalieni mpapai unayoosha miguu juu , alikua kama amepagawa ila baadae alitulia sahivi kaacha jumla mwaka kama wa 9 huu hanywi pombe
 
Nami niliacha pombe ghafla baada ya kupata kashfa babkubwa itokanayo na kilevi.

Niliitumia pombe almost 20yrs na nilivyojikatili kuacha sikupata madhara yoyote mpaka leo miaka 30 sasa.

Hayo unayodai sijui mishipa kufanyaje, hali hiyo mi'haikunipata.

Kilichoniathiri baada ya kuacha ni kukosa cha kufanya ili kucover masaa niliyoyatumia matembezini na bar.

Nikawa najiuliza: nisipotoka niwe baba wa nyumbani au, ni mtihani kwa kweli!

Huo ndiyo mtihani mkubwa, usipoangalia hali hiyo yaweza kukurejesha majaribuni.

Nilichokifanya ni kufungua project ya kilimo kwa kununua shamba pori na kuanza kulisafisha mwenyewe bila kuweka kibarua ili kujikeep buse na ilinisaidia!

Kusafisha shamba hadi kuchimba visiki kwa ekari 8 kwa kufanya kazi kila nipatapo muda nilipotoka kazini, nilitumia kama miaka mitatu na muda huo pombe ikawa imeisha mwilini na kuisahau kabisa.

Ndoto za kuota nipo bar ziliendelea kuniandama zaidi ya miaka10!

Bwana mzee kuacha pombe ni maamuzi ya busara na hakuna madhara zaidi ya faida.
 
Pombe haina faida ndugu zangu zaidi ya hasara tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…