Hivi Kuna madhara ya kuweka pombe Kali kwenye fridge na baadae kuinywa??

hilo swali ungeuliza huko bar ni kwanini hivyo vinywaji ulivyotaja wao huko bar hawaviweki kwenye friji watakupa jibu sahihi..ila mm nasikia tu hivyo vinywaji vikali havitakiwi kukaa kwenye friji zipo sababu maalum za kitaalam ila mm sizijui..labda walevi na wafanyabiazhara wa hizo pombe watujuze ni kwanini.? ila wengine wanaweka vpande vya barafu kwenye glasi za pombe kali sijui nayo iko vipi.!
 
Je ukiweka petroleum,Yai, Spirit ya vidonda kwenye friji navyo vina Ganda vinakua barafu. Na Kama Yai liki Ganda je litakua Kama lime chemshwa.😂😂😂😂🙌🙌🙌
 
Nazungumzia pombe Kali kama; K-vant,konyagi, grants, smin off, jack Daniels nk nk.

Nauliza Kuna mlevi Mmoja hapa Jf alishawahi kujaribu hii challenge??, na Nini kilitokea??, Natamani kujua hili......tchao!!!
Acha maisha ya ulevi, mwanangu. Mungu sio mjomba wako. Hujasoma onyo lake?
Soma 1 Wakorintho 6:9-10
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi, hawataurithi ufalme wa Mungu."
 
Acha ku judge mkuu sawa??....una judge mtu alafu mwisho wa siku hoja Yako ya msingi ni kama yangu TU,, tulia watiririke tupate majibu
 
Nazungumzia pombe Kali kama; K-vant,konyagi, grants, smin off, jack Daniels nk nk.

Nauliza Kuna mlevi Mmoja hapa Jf alishawahi kujaribu hii challenge??, na Nini kilitokea??, Natamani kujua hili......tchao!!!
Nimeuliza robot na haya ndio majibu yake:
"Ndio, unaweza kuweka pombe kali kama Konyagi na K-Vant kwenye friji ili zipate ubaridi. Pombe kali zina kiwango cha juu cha alkoholi (kawaida zaidi ya 30%), hivyo haziwezi kuganda kwenye friji ya kawaida kwa sababu kiwango cha kuganda cha alkoholi kiko chini sana (karibu -114°C).

Hata hivyo, ikiwa unataka zipate ubaridi wa haraka zaidi, unaweza pia kuweka kwenye freezer kwa muda mfupi (dakika 20–30). Kumbuka tu kuwa pombe kali hazitaganda kwenye freezer ya kawaida kwa sababu ya kiwango chake cha juu cha alkoholi."
 
Wapi mkuu nimetaja Mimi mlevi??,, kabla ya ku judge mtu ji judge ww mwenyewe kwanza sawa?
 
Muulize huyo robot wako, Vipi tunachelewa au tunawahi kulewa, hiyo ndio hoja ya msingi....ndio jibu AMBALO walevi wanatamani kulijua
 
Muujiza wa kwanza wa yesu kristo ulikua upi ndugu mtumishi??

Kina lutu ambao walikua wanaongea na malaika live walikua wanapiga vyombo mpaka wamelala na Binti zao .
 
Muulize huyo robot wako, Vipi tunachelewa au tunawahi kulewa, hiyo ndio hoja ya msingi....ndio jibu AMBALO walevi wanatamani kulijua
"Ubaridi hautabadili kiwango cha alkoholi kwenye pombe, kwa hiyo hali ya kulewa itabaki ile ile. Kilichobadilika ni ladha na hisia unazopata unapokunywa — pombe ikiwa baridi huwa laini zaidi na ladha yake huwa nyepesi, hivyo inaweza kukufanya unywe kwa kasi zaidi bila kuhisi ukali wake mara moja. Hii inaweza kusababisha kulewa haraka bila kujitambua kwa sababu unywaji unakuwa rahisi zaidi."

Mwisho wa kunukuu. Kula vyombo
 




Sira 31​


27😛ombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi.
Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29Lakini kunywa pombe kupita kiasi,
kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha.
30Ulevi huongeza hasira ya mpumbavu akajiumiza mwenyewe;
humdhoofisha na kumwongezea majeraha.
31Usimkaripie jirani yako kwenye pombe,
wala usimdharau anapofurahia karamu.
Usimwambie neno la kumwonya,
wala usimsumbue kwa kumtaka alipe deni....."Kila Kitu Ni Kwa Kiasi Na Wakati"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…